Serikali inakusudia kupeleka bungeni muswada wa sheria ya mabadiliko kwa watumishi wa tasnia ya habari ili kukuza uweledi wa taaluma hiyo.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye ameiambia Star tv kuwa pamoja na masuala mengi muswada huo utatazama juu ya sifa za kufuzu kuwa Mwandishi wa Habari.

Miongoni mwa sifa hizo ni pamoja na kuhitimu shahada kama hatua ya kuhakikisha Mwaandishi wa Habari wanabobea katika masuala wanayoyaandika.

Waziri Nape ametoa kauli hiyo baada ya kuhitimisha ziara yake katika ofisi za kampuni ya Sahara Media Group ambapo ametembelea kujionea namna vituo vya utangazaji wa Star Tv, Radio Free Africa na Kiss Fm vinavyorusha matangazo yake.

 

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here