Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kimataifa

Kimataifa

Habari za Kimataifa kutoka Star TV. Pata Habari za ulimwenguni kote katika nyanja za; siasa, uchumi, utamaduni, michezo.

TETEMEKO LA ARDHI.

Kumetokea  tetemeko  kubwa  la  ardhi  nchini New Zealand  likiwa  na  kipimo  cha  6.2  mzani  wa Ritcher  mapema  limetanguliwa  na  lingine  lenye  kipimo  cha  7.8 mzani  wa Ritchter  kwa  pamoja  yameacha  hasara  kubwa  ikikadriwa  kugharimu  mamilioni  ya Dola.

Soma Zaidi

Obama awataka wakuu wa Republican wajitenge na Trump

  Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito kwa viongozi wakuu wa chama cha Republican kuondoa rasmi uungaji mkono wao kwa mgombea wa chama hicho Donald Trump.   Akiongea katika mkutano wa kampeni wa kumuunga mkono mgombea wa chama cha Democratic Hillary Clinton, Bw Obama amesema haina maana kukemea matamshi …

Soma Zaidi

Video ya raia wa Uganda akiuwawa na polisi Marekani yatolewa

Polisi katika mji wa Marekani San Diego wametoa mkanda wa video ya mwanamme mweusi aliyepigwa risasi na kuuwawa na polisi siku ya jumanne. Video hiyo inaonyesha maafisa wawili wa polisi wakimkaribia Alfred Olango – mkimbizi kutoka Uganda – ambaye hakuwa amejihami, kabla ya mmoja wao kumfyatulia risasi katika mtaa wa …

Soma Zaidi

Marekani na Urusi zatupiana maneno juu ya Syria

Marekani na Urusi zimelaumiana vikali kwenye baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya mashambulizi dhidi ya msafara wa misaada nchini Syria, pamoja na hatua ya kuvunja mkataba wa kusitisha mapigano. Wamarekani wamekuwa wakiamini kuwa Urusi ndio iliyoshambulia msafara huo, huku Warusi wakilipinga hilo. Waziri wa Mambo ya Nchi …

Soma Zaidi

Mshukiwa wa shambulio New York alisifu Islamic State

Waendesha mashtaka nchini Marekani wamemfungulia mashtaka Ahmad Khan Ramani kwa kutega mabomu huko New York na New Jersey mwishoni mwa wiki ambapo mlipuko mmoja ulijeruhi watu 31. Waendesha mashtaka wanasema kuwa Bw Rahami ambaye ni mhamiaji kutoka Afghanistan, alinunua vifaa na vitu vya kuunda bomu kupitia kwa mtandao na kuandika …

Soma Zaidi

Marekani yaitupia lawama Urusi, shambulio la Syria

Marekani imesema ndege za kivita za Urusi zilihusika kushambulia msafara wa misaada nchini Syria siku ya Jumatatu na kusababisha vifo. Maafisa wa Marekani wameiambia BBC ndege mbili za kivita za Urusi aina ya SU-24, zilikuwa angani, sambamba na msafara huo wa magari, wakati tukio hilo likitokea. Hata hivyo Urusi imekana …

Soma Zaidi

George HW Bush kumpigia kura Clinton

Aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani kupitia tiketi ya chama cha Republican George HW Bush amesema kuwa atampigia kura mgombea wa urais kupitia tiketi ya Democrat Hillary Clinton. Bwana Bush amedaiwa kutoa ahadi hiyo kwa Kathleen Kennedy Townsend, mpwa wa rais wa zamani nchini humo John F Kennedy. Afisi ya …

Soma Zaidi