Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Kimataifa (Ukurasa 10)

Kimataifa

Habari za Kimataifa kutoka Star TV. Pata Habari za ulimwenguni kote katika nyanja za; siasa, uchumi, utamaduni, michezo.

Obama atahadharisha juu ya ugaidi wa silaha za nyuklia

Katika mkutano wa kilele kuhusu usalama wa nyuklia huko mjini Washington, Rais wa Marekani Barack Obama ametahadharisha juu ya watu aliyowaita “wandawazimu” akimaanisha magaidi wa kundi linalojiita dola la kiislamu IS, kuwa wanaweza kufanya  janga  la shambulizi kwa  kutumia silaha za nyuklia bila ya kusita. Rais Obama ambaye anatarajiwa kuondoka …

Soma Zaidi

Zuma akubali makosa kuhusu ukarabati Nkandla

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amekubali uamuzi wa Mahakama ya Kikatiba uliompata na hatia kuhusiana na ukarabati uliofanywa katika makao yake ya kibinafsi eneo la Nkandla. Akihutubia taifa hilo moja kwa moja kupitia runinga, Bw Zuma amesifu mahakama hiyo na kusema imedhihirisha kuwepo kwa uhuru wa mahakama nchini humo. …

Soma Zaidi

Kenya Airways kuwafuta kazi wafanyikazi 600

Wafanyikazi 600 wa Shirika la Ndege la Kenya, Kenya Airways watapoteza kazi zao katika juhudi za kulichepua shirika hilo. Kenya Airways ilitangaza hasara ya dola milioni 270 mwaka uliopita, ikiwa ndio hasara kubwa zaidi kuripotiwa na kampuni nchini Kenya. Makali ya hasara yalioripotiwa na kampuni hiyo sasa yameanza kuwalenga wafanyikazi …

Soma Zaidi

Serikali ya Burundi  yakana Madai ya ukiuka wa haki za binadamu:

Bunge la Afrika mashariki linaloendelea jijini Arusha na kusikiliza utetezi kutoka serikali ya nchi ya Burundi iliyotakiwa kujibu madai kutoka kwa asasi za kiraia na taasisi za kisheria, juu ya mauaji na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini humo. Hatua hiyo imefikiwa ikiwa ni matokeo ya madai yaliyopelekwa na …

Soma Zaidi

Hali Ya Kisiasa Burundi  Serikali ya Burundi yakubali usuluhishi

  Rais John Magufuli amefanya mazungumzo na Spika wa Seneti na Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Burundi Reverien Ndikuriyo Ikulu jijini Dar es Salaam kuhusu hali ya kisiasa na usalama nchini Burundi na jitihada zinazochukuliwa na Tanzania ikiwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Akiwasilisha ujumbe wa …

Soma Zaidi

Mshambulizi Paris atajwa kuwa ni Omar Mostefai

Mshambulizi Paris atajwa:Omar MostefaiWaendesha mashtaka wanaouchunguza matukio ya mashambulio ya kigaidi mjini Paris Ufaransa wamemtaja mmoja wa washambuliaji 7 wa kujitoa mhanga. Omar Ismail Mostefai mwenye umri wa miaka 29 anasemekana kuwa ni raia wa ufaransa aliyekuwa anachunguzwa na polisi wa kupamabana na ugadi kabla hajatoweka. Mtu huyo tayari alikuwa …

Soma Zaidi

Gari la pili la wavamizi lapatikana Paris

Gari la pili lililotumika na wavamizi lapatikana ParisPolisi wa Ufaransa wamelipata gari la pili linalofikiriwa lilitumika katika mashambulio ya Ijumaa usiku mjini Paris. Gari hilo la aina ya Seat, lilipatikana limeachwa mashariki mwa jiji. Aidha gari hilo liinavoripoitiwa lilikuwa na silaha. Awali gari lilokodiwa Ubelgiji, lilipatikana hapo jana, karibu na …

Soma Zaidi

Askari Sudan wadaiwa kuua na kubaka raia

Kikosi kimoja maalum cha serikali nchini Sudan kimeshutumiwa kwa kutekeleza maujai ya halaiki na ubakaji wa raia katika eneo la Darfur Magharibi tangu mwezi Februari mwaka uliopita. Ripoti mpya ya Shirika la kutetea haki za Kibinadamu Human Rights Watch inasema kikosi hicho kijulikanacho kama Rapid Support Forces kilitekeleza kile inachosema …

Soma Zaidi

Majaji 34 Ghana kuhojiwa kwa kula rushwa

Uchunguzi uliofanywa na mwandishi habari za uchunguzi , Anas Aremeyaw Anas uliomchukua miaka miwili umegundua kuwa majaji pamoja na viongozi wa juu wa mahakama nchini humo wanakula rushwa . Mwandishi huyo wa habari Anas tayari amekwisha waandikia waraka Rais wa nchi hiyo pamoja jaji mkuu ambao nao tayari wamekwisha andaa …

Soma Zaidi