Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Kimataifa (Ukurasa 20)

Kimataifa

Habari za Kimataifa kutoka Star TV. Pata Habari za ulimwenguni kote katika nyanja za; siasa, uchumi, utamaduni, michezo.

Merkel ataka suluhu kwa mazungumzo.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel,amesema kwamba historia inatoa funzo la umuhimu wa kupata suluhu ya migogoro ya aina mbali mbali kwa njia ya majadiliano. Akiongea na waandishi wa habari Kansela Angela Merkel alisisitiza umuhimu wa mkataba wa amani kuhusu Ukraine kuandaliwa. Mapema kiongozi huyo wa Ujerumani aliweka shada la maua …

Soma Zaidi

Rais wa zamani wa Uturuki afariki dunia

Aliyekuwa rais wa Uturuki Kenan Evren ambaye aliongoza mapindunzi yaliyokumbwa na umwagikaji wa damu mwaka 1980 ameaga dunia kwenye hospitali moja mjini Ankara akiwa na umri wa miaka 97. Mwaka uliopita alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kufuatia kuhusika kwake kwenye mapinduzi ya kijeshi. Chini ya utawala wake watu kadha walinyongwa …

Soma Zaidi

Mashambulizi zaidi yafanyika Yemen.

Vikosi vinavyoongozwa na Saudi Arabia vimeendesha mashambulizi kwenye mjii mkuu Yemen sanaa vikilenga nyumba ya rais wa zamani Ali Abdullah Saleh. Milipuko mikubwa ilisikika na moshi mkubwa ulionekana ukitanda angani kutoka eno hilo. Rais huyo wa zamani ni mshirika wa waasi wa Houthi ambao wanaendesha harakati za kutaka kuidhibiti Yemen. …

Soma Zaidi

Waandamanaji wapewa saa 48 Burundi

Serikali ya Burundi imewaagiza waandamanaji katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura kusitisha maandamano yao dhidi ya hatua ya rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwezi ujao. Mamlaka imewapatia waandamanaji hao saa 48 kuondoa vizuizi walivyoweka katika barabara za mji huo. Hakuna maandamano yanayoendelea …

Soma Zaidi

Baada ya kushindwa, Viongozi wa upinzani wajiuzulu Uingereza.

Kiongozi wa chama cha Leba nchini Uingereza Ed Miliband amewaambia wanaharakati wa chama hicho kwamba anajiuzulu kama kiongozi wa chama hicho kufuatia matokeo duni ya uchaguzi mkuu. Miliband ambaye amempongeza Waziri mkuu David Cameron kwa kuchaguliwa kwa awamu ya pili amesema kuwa anachukua jukumu la kushindwa kwa chama chake katika …

Soma Zaidi

John Kerry azuru mji wa Mogadishu

Waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewasili katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu ambapo anakutana na rais Hassan Sheikh Mohamud,viongozi wa eneo la Afrika mashariki pamoja na mashirika ya kijamii. Ni waziri wa kwanza wa kigeni kutoka Marekani kuutembelea mji huo. Kerry hataondoka katika uwanja wa ndege …

Soma Zaidi

Mahakama yaruhusu Nkurunziza kuwania urais

Mahakama ya kikatiba nchini Burundi imemruhusu rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu. Kulingana na vituo vya redio nchini humo,Jaji wa mahakama hiyo alitoa uamuzi huo mapema leo asubuhi . Hapo Jana makamu wa mahakama hiyo Jaji Sylvere Nimpagaritse ,alilitoroka taifa hilo akidai kuwa walikuwa wakishinikizwa kutoa uamuzi utakaompendelea rais …

Soma Zaidi

Netanyahu ashtumu ubaguzi Israeli

Waziri mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameelezea mshangao wake binafsi kwa mwanajeshi wa Israeli wa asili ya Ethiopia ambaye alipigwa na polisi wa Israeli hali iliyosababisha kutokea kwa maandamano. Bwana Netanyahu alimuambia Damas Fikadeh kuwa kitendo hicho hakikubaliki, na madabiliko yanahitaji kufanywa. Maandamano IsraelBwana Fikadeh alisema alitiwa moyo na matamshi …

Soma Zaidi

Watu 3 wauawa katika maandamano Burundi.

Takriban watu wawili wameuawa wakati wa ghasia kati ya polisi na waandamanaji kwenye mji mkuu wa Burundi Bujumbura . Polisi walifyatua risasi huku waandamanaji wakirusha mawe na guruneti. Ghasia BurundiPolisi wawili na waandamanaji sita nao walijeruhiwa. Waandamanaji hao wanalalamikia hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania urais kwa muhula wa …

Soma Zaidi

Mateka wasimulia mateso ya Boko Haram

Wanawake na watoto waliokuwa wakishikiliwa mateka na kikundi cha Kiislam cha Boko Haram kaskazini mwa Nigeria wamesema baadhi yao waliuawa kwa kupigwa mawe na wapiganaji wa Boko Haram wakati jeshi lilipokaribia kuwaokoa. Walikuwa wakizungumza siku moja baada ya karibu mateka mia tatu kuokolewa kutoka msitu wa Sambisa na kuwapeleka katika …

Soma Zaidi