Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kimataifa (Ukurasa 3)

Kimataifa

Habari za Kimataifa kutoka Star TV. Pata Habari za ulimwenguni kote katika nyanja za; siasa, uchumi, utamaduni, michezo.

Maafisa 4 wa polisi washtakiwa kwa mauaji Kenya

Maafisa 4 wa polisi wa kituo cha Syokimau Kenya wanaotuhumiwa kwa mauaji ya wakili mmoja na mteja wake pamoja na dereva wao wa teksi wamekanusha mashtaka dhidi yao. Maafisa hao sajini wa polisi wa utawala Fredrick Leliman,na Leonard Maina Mwangi, pamoja na koplo wa polisi Stephen Chebulet na konstebo Silvia …

Soma Zaidi

Polisi 8,000 wasimamishwa kazi Uturuki

Vikosi vya usalama nchini Uturuki vinasema kuwa zaidi ya maafisa 8,000 wa polisi wamefutwa kazi, kufuatia jaribio la mapinduzi lililozimwa wiki iliyopita. Runinga rasmi ya serikali nchini Uturuki- Anadolu, inasema kuwa maafisa wengine waliokamatwa ni pamoja na majenerali wakuu wa kijeshi. Takriban wanajeshi elfu 6,000 na wahudumu wa mahakama nao …

Soma Zaidi

Washukiwa 3 wa shambulizi wakamatwa Ufaransa

Polisi nchini Ufaransa wamewakamata watu watatu wanaohusishwa na shambulizi la lori la siku ya Alhamis mjini Nice lililosababisha vifo vya watu 84. Wale waliouawa walikuwa kati ya umati mkubwa uliokuwa ukitizama maonyesho ya fataki, wakati lori lilivurumishwa makusudi kwenda eneo walikuwa. Zaidi ya watu 50 wako hali mahututi hospitalini. Siku …

Soma Zaidi

Shambulio laua watu zaidi ya 80 Ufaransa

Zaidi ya watu 80 wameripotiwa kuuawa katika shambulio lililotokea katika mji wa Nice kusini mwa Ufaransa. Lori lililokuwa likienda mwendo kasi lilijiingiza katika mkusanyiko wa watu waliokuwa wakiangalia maonesho ya fataki kuadhimisha siku ya kitaifa ya Bastille, ambayo huja na shamra shamra kila mwaka. Mwendesha mashtaka katika mji wa Nice, …

Soma Zaidi

Al shabab waua maafisa 4 wa polisi Kenya

Maafisa wanne wa polisi wanahofiwa kufariki baada ya mtu mshukiwa wa ugaidi kumpokonya askari bunduki na kuwafyatulia maafisa wa Polisi. Yamkini mshukiwa huyo wa ugaidi alikuwa amefungiwa korokoroni baada ya kukamatwa kwa tuhuma za kujaribu kuwashawishi watu kujiunga na mtandao wa kigaidi wa Al Shabaab. Alipelekwa katika kituo cha polisi …

Soma Zaidi

Mbunge wa bunge la afrika mashariki Hafsa Mossi auawa Burundi

Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki kutoka Burundi Hafsa Mossi ameuawa na watu wasiojulikana mjini Bujumbura. Bi Mossi, aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki katika serikali ya nchi hiyo, aliuawa kwa kupigwa risasi katika barabara ya Gihosha, eneo la Nyankoni. Mbunge huyo aliwahi kufanya kazi na idhaa …

Soma Zaidi

Foleni ya magari yauwa watu 12

Wengi walifariki kutokana na kukosa maji mwilini na uchovu. Watu wengi waliokuwa wakisafiri kwa sherehe za kuadhimisha mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhan walikusanyika katika makutano ya barabara kisiwa cha Java. Na hapo ndipo msongamano mkubwa wa magari ulipotokea.   Maafisa wa uchukuzi nchini Indonesia wanasema vifo hivyo vimetokea katika …

Soma Zaidi

Donald Trump amsifu Saddam Hussein

Mgombea urais wa chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amemsifu kiongozi wa zamani wa Iraq Saddam Hussein akisema aliweza kukabiliana vyema na magaidi. Bw Trump alikuwa akihutubia mkutano wa kampeni eneo jimbo la North Carolina Jumanne alioanza kuzungumza kuhusu kiongozi huyo aliyeuawa kwa kunyongwa Desemba 2006. “Saddam Hussein alikuwa …

Soma Zaidi

Tembo wavamia mashamba ya chakula Uganda

Ndovu kutoka mbuga ya Nimule nchini Sudan Kusini wamekuwa wakivuka na kuingia Kaskazini mwa Uganda na kuharibu mashamba ya mahindi , mihogo , viazi na pamba Maurice Vuzi ambaye ni mwenyekiti wa wa kaunti ndogo ya Dufile, alisema kuwa ndovu hao waliharibu zaidi ya ekari 35 ya mimie siku ya …

Soma Zaidi