Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Kimataifa (Ukurasa 30)

Kimataifa

Habari za Kimataifa kutoka Star TV. Pata Habari za ulimwenguni kote katika nyanja za; siasa, uchumi, utamaduni, michezo.

Indonesia wakumbuka Tsunami.

Wananchi wa Indonesia wameanza kuadhimisha mwaka wa kumi tangu kutokea kwa tetemeko la ardhi lililosababisha mawimbi makubwa katika bahari ya Hindi, tsunami na kusababisha vifo vya watu zaidi ya watu laki mbili na elfu ishirini katika eneo kubwa. Umati wa watu umekusanyika karibu na jengo la makumbusho la tsunami katika …

Soma Zaidi

Sudan yawatimua maafisa wa UN.

Umoja wa mataifa unasema kuwa Sudan imewafukuza maafisa wake wawili wakuu kutoka nchini humo. Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Ban Ki-moon, amelishutumu taifa hilo kwa kumfurusha mshirikishi mkuu wa utoaji msaada Ali Al-Zatari, na mkurugenzi mkuu wa mpango wa maendeleo wa Umoja wa mataifa Nchini humo Yvonne Helle. Haijafahamika …

Soma Zaidi

Polisi auawa Kenya.

Askari mmoja ameuawa na mwingine akiwa mahututi baada ya kushambuliwa kwa kupigwa risasi kaskazini mwa Kenya. Askari hao wa Kenya wanadaiwa kushambuliwa na watu wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa kundi la Al Shabaab. Askari hao wa jeshi la polisi kikosi cha ziada walikutwa na kisa hicho mjini Wajir kaskazini mwa …

Soma Zaidi

Rais wa Ufaransa awatuliza raia wake.

Rais wa Ufaransa amewataka raia wake wasishtushwe na visa vya kushambuliwa kwa polisi na raia katika kipindi cha siku kadhaa. Rais Francois Hollande ameyasema hayo baada ya mtu mmoja kuendesha gari na kulivurumisha katika soko la Krismasi lililosheheni watu, magharibi mwa mji wa Nantes na kujeruhi watu kumi. Waendesha mashtaka …

Soma Zaidi

Somalia yawakataa wanajeshi wa Sierra Leone

Wanajeshi wa kulinda amani kutoka Sierra Leone wameondoka nchini Somali na hakuna wanajeshi wengine wa taifa hilo watakaochukua mahala pao kufuatia wasiwasi wa ugonjwa wa Ebola. Umoja wa Afrika una mpango wa kutafuta wanajeshi wengine kutoka mataifa yenye wanajeshi wake nchini humo. Zaidi ya wanajeshi 800 wa Sierra Leone walio …

Soma Zaidi

Marekani yaitupia lawama Korea Kaskazini.

Marekani inatarajia kuirudisha Korea kaskazini katika orodha ya nchi zinazofadhili ugaidi. Rais Barack Obama wa Marekani amesema utawala wake utafanya hivyo baada ya kuilaumu nchi hiyo kufanya uhalifu wa mtandao dhidi ya kampuni ya Sony Pictures. Amesema mara tu mchakato wao huo utakapokamilika, watajibu mashambulizi hayo. Korea kaskazini imeziita tuhuma …

Soma Zaidi

Essebsi ajitangaza kushinda Tunisia.

Matokeo ya awali ya uchaguzi wa Rais nchini Tunisia yanaonesha kuwa Beji Caid Essebsi anaongoza kwa zaidi ya asilimia 55 ya kura Licha ya Kujitangaza mshindi, mpinzani wake ambaye ameshika nafasi ya pili Moncef Marzouki amesema matokeo hayo yanakaribiana mno. Wakati wafuasi wa Beji Caid Essebsi wakishangilia ushindi, kiongozi wa …

Soma Zaidi

Wafungwa wakutwa wakila raha gerezani.

Polisi mjini Manila wamevamia gereza moja na kuushangaza umma wa Philippines baada ya kung’amua maisha ya anasa yanayoendelea ndani ya gereza hilo kwa kikundi cha baadhi ywa wafungwa wenye upendeleo wa kipekee. Uvamizi huo umefanywa katika gereza hilo la Bilibid lenye wafungwa wengi nchini humo kufuatia taarifa kwamba mtandao wa …

Soma Zaidi

Ocampo: Nilikuwa sahihi kumshitaki Kenyatta.

Kiongozi wa zamani wa mashitaka katika mahakama ya jinai ya ICC, ameteta uamuzi wake wa kumshitaki Rais Uhuru Kenyatta licha ya kesi hiyo kutupiliwa mbali. Bwana Luis Moreno Ocampo anasema kua mashitaka hayo dhidi ya Uhuru yalizuia ghasia kutokea tena katika uchaguzi wa mwaka 2013. Kenyatta alishinda uchaguzi huo baada …

Soma Zaidi

Idadi ya waliouawa Pakistan yafika 130.

Vikosi vya usalama nchini Pakistan vinakabiliwa na hali ngumu kuweza kudhibiti shule iliyovamiwa na wapiganaji wa Taliban katika jimbo la Peshawar Kaskazini Magharibi mwa Pakistan Takriban watu miamoja na thelathini wamefariki , wengi wao wakiwa watoto. Msemaji wa jeshi anasema washukiwa sita wameuawa huku operesheni hio ikiendelea. Shule hio inasimamiwa …

Soma Zaidi