Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Kimataifa (Ukurasa 49)

Kimataifa

Habari za Kimataifa kutoka Star TV. Pata Habari za ulimwenguni kote katika nyanja za; siasa, uchumi, utamaduni, michezo.

Obama akutana na rais Zuma

Rais wa Marekani Barack Obama, amesema uvumilivu na ujasiri wa Nelson Mandela ni mfano mwema kwa dunia na upendo wa dhati wa rais huyo wa zamani wa taifa la Afrika Kusini inaonyesha ni kwa namna gani alivyo na utu wa kibinadamu. Bwana Obama ameongeza kuwa Mandela, alionyesha ukweli na ukakamavu …

Soma Zaidi

Mauaji Misri , Watu kumi wauawa Kismayo

Wakaazi wa mji wa Kusini wa Somalia Kismayo wanaendela kukikmbia makwao, kutokana na mapigano makali kati ya mababe wa kivita katika eneo hilo. Takriban raia kumi wameuawa katika mapigano hayo yaliyotokea siku ya Ijumaa. Mji wa Kismayo ni mji muhimu wa kiuchumi Kusini mwa Somalia na vita hivyo vimechochewa na …

Soma Zaidi

Marekani yatoa onyo kwa raia wake Misri

Serikali ya Marekani imetoa tahadhari kwa raia wake kutosafiri nchini Misri huku ikiwataka maafisa ambao hawajaajiriwa katika ubalozi wake nchini humo kuondoka mara moja kutokana na ghasia zinazoendelea . Baadhi ya raia wamefariki huku wengine wengi wakijeruhiwa vibaya kufuatia makabiliano kati ya wafuasi wa rais Mohammed Morsi na wale wa …

Soma Zaidi

Rais Morsi aonya dhidi ya maandamano

Rais wa Misri Mohammed Morsi ameonya kuwa vurugu za siasa zinaathiri demokrasia nchini humo. Katika hotuba ya taifa kupitia televisheni kuadhimisha mwaka mmoja tangu achukue uongozi, Bw Morsi alikiri kuwa amefanya makosa kadhaa. Kadhalika aliutaka upinzani kuwasilisha matakwa yake kupitia kura. Hata hivyo uongozi wake umekumbwa na changamoto si haba …

Soma Zaidi

Obama asifu Senegal kwa demokrasia

Rais wa Marekani Barack Obama ambaye yuko katika ziara yake ya Afrika, amesifu nchi ya Senegal kwa kuwa moja ya nchi zenye demokrasia thabiti barani Afrika. Akiwahutubia waandishi wa habari nchini Senegal kwa mkondo wake wa kwanza wa ziara yake Afrika,baada ya mazungumzo na rais Macky Sall, Bwana Obama alisema …

Soma Zaidi

Familia ya Mandela yakosoa wanahabari.

Taarifa kutoka Ikulu ya Afrika Kusini zinasema kuwa hali ya kiafya ya rais mstaafu Nelson Mandela sio nzuri na kuwa imezorota katika saa 48 zilizopita. Baada ya kumtembelea hospitalini, mwanawe mkubwa wa kike Makaziwa, alisema hali inaonekana kuwa mbaya lakini akaongeza kuwa Mandela anaweza kuwasikia jamaa zake wanapomuita huku akijaribu …

Soma Zaidi

Tsvangirai apingana na Mugabe kuhusu uchaguzi

Waziri mkuu nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ametoa wito kwa mahakama ya kikatiba nchini humo kufutilia mbali agizo la rais wa taifa hilo Robert Mugabe kuandaa uchaguzi mwishoni mwa mwezi Julai. Tsvangirai ameonya kuwa huenda taifa hilo likakumbwa na hali ya switofahamu iwapo uchaguzi huo utafanyika. Katika ombi lake waziri huyo …

Soma Zaidi

4 wanyongwa nchini Nigeria

Wafungwa wanne wamenyongwa kusini mwa Nigeria, katika kile maafisa wanasema kuwa hukumu ya kwanza ya kunyongwa kutekelezwa kwa miaka saba. Kamishna wa haki katika jimbo la Edo, Henry Idahagbon, aliambia waandishi wa habari kuwa wafungwa hao walinyongwa baada ya kuhukumiwa kifo kwa makosa ya wizi wa mabavu na mauaji. Shirika …

Soma Zaidi

37 wafariki kwenye machimbo CAR

Wachimba migodi 37 wameuawa baada ya mvua kubwa kusababisha kuporomoka kwa machimbo walimokuwa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati. Maafisa wanasema kuwa ajali hiyo ilitokea Jumapili karibu na mji wa Ndassima, umbali wa kilomita 440 Mashariki mwa mji mkuu,Bangui. Kwa mujibu wa msemaji wa serikali, siku tatu za kuomboleza zimetangazwa …

Soma Zaidi

Mzee Mandela bado yuko hali mahututi

Rais mstaafu wa Mandela Nelson Mandela, bado yuko hali mahututi ingawa madaktari wanadhibiti hali yake baada ya afya yake kuzorota mwishoni mwa wiki. Taarifa kutoka ikulu ya rais zinasema kuwa Mandela angali yuko chini ya uchunguzi wa madaktari ambao wameweza kuidhibiti hali yake. Anaugua maradhi ya mapafu na amelazwa hospitalini …

Soma Zaidi