Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Kimataifa (Ukurasa 5)

Kimataifa

Habari za Kimataifa kutoka Star TV. Pata Habari za ulimwenguni kote katika nyanja za; siasa, uchumi, utamaduni, michezo.

Al shabaab waua polisi 5 Mandera Kenya

Maafisa 5 wa polisi wa Kenya wameuawa mapema leo mjini Mandera katika shambulizi lililotekelezwa na wapiganaji wa kundi la wanamgambo la Al shabab kutoka Somalia. Kamishna wa jimbo hilo la kaskazini mashariki mwa Kenya bwana Job Borongo ameithibitishia BBC kuwa wapiganaji hao walifanya shambulizi la kuvizia dhidi ya msafara wa …

Soma Zaidi

Redio na TV zafunga matangazo DRC kisa hiki hapa

Baadhi ya vituo vya redio na runinga katika mji mkuu Kinshasa, katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, zimefunga matangazo yake kuanzia leo, ikiwa ni ishara ya kuanza mgomo kufutia makampuni ya simu za mikononi kupandisha gharama za huduma za intaneti. Ni karibu majuma matatu sasa, tangu gharama ya huduma hiyo …

Soma Zaidi

Wanajeshi wa Iraq waukomboa mji wa Fallujah kutoka kwa IS

Waziri mkuu wa Iraqi, Haider al Abadi, ametangaza kuwa mji wa Faluja umekombolewa na wanajeshi wa Serikali. Katika taarifa fupi aliyoitoa kwa runinga ya kitaifa moja kwa moja, bwana Abadi alisema kuwa makundi machache ya wapiganaji wa Kiislamu wenye itakadi kali wa Islamic State wangali Falujjah, lakini akawahakikishia wananchi kuwa …

Soma Zaidi

Mwanajeshi awaua watu 8 kwenye kambi nchini Uganda

Jumla ya watu wanane wameuawa baada ya kupigwa risasi ndani ya kambi ya kijeshi ya Makindye mjini kampala nchini Uganda Msemaji wa jeshi la Uganda meja Edward Birungi, anasema kuwa mwanajeshi huyo anaripotiwa kutofautiana na mkewe. Anaripotiwa kuwa mlevu na alikuwa pia amevuta bangi akiwa kazini, ambapo alianza kufyatua risasi …

Soma Zaidi

Mabaki ya EgyptAir yapatikana

Mamlaka ya Misri inasema mabaki ya ndege ya EgyptAir ambayo ilianguka katika bahari ya Mediteranian mwezi uliopita ikiwa imebeba abiria sitini na sita yameweza kubainika yalipo. Katika maelezo yaliyotolewa na kamati husika ya uchunguzi wa ajali hiyo wanasema ,meli inayotafuta mabaki ya ndege ya EgyptAir imeweza kubaini maeneo kadhaa ambayo …

Soma Zaidi

Besigye afikishwa mahakamani tena

Jaji nchini Uganda ametoa amri kuwa kesi ya kiongozi wa upinzani nchini humo Kizza Besigye, ifanyike mahakamani kwa makosa ya uhaini na wala sio kwenye gereza lenye ulinzi mkali ambapo anazuiliwa. Besigye alifikishwa mahakamani kwa muda mfupi ambapo kesi yake iliahairisha hadi tarehe 29 mwezi Juni. Mwendesha mashtaka aliomba kesi …

Soma Zaidi

Obama amshtumu Trump kuhusu kuwazuia Waislamu kuingia nchini marekani

Rais wa Marekani, Barack Obama, ameshtumu vikali matamshi ya mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwamba waislamu wasiruhusiwe kuingia Marekani. Obama amesema hiyo ‘si marekani wanayohitaji.’ ”Kuwabagua Waislamu wa Marekani kutasababisha nchi hiyo kukosa usalama,na kuongeza tofauti iliopo kati ya nchi za magharibi na zile za …

Soma Zaidi

Ndege yenye maadili ya Kiislamu yapigwa marufuku Malaysia

Shirika la ndege la Malaysia, Rayani Air, linalozingatia misingi ya dini ya kiislamu katika biashara zake, limepigwa marufuku na idara ya safari za ndege nchini humo baada ya ukaguzi kuonyesha halijakidhi viwango na vigezo vya kiusalama. Rayani Air ilianzishwa Disemba ikinadi kuendeleza desturi za kiislamu katika huduma zao zote zikiwemo …

Soma Zaidi