Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa (Ukurasa 30)

Kitaifa

Habari za Kitaifa, Tanzania bara na visiwani (Zanzibar).

Baadhi ya wazazi Monduli wakataa kuchangia michango Shuleni.

  Baadhi ya wazazi wilayani Monduli mkoani Arusha wamekataa kuchangia michango yote ya shule wakidai kuwa Rais Magufuli amewataka wasichangie katika agizo lake la elimu bure. Ni katika ziara ya mbunge wa jimbo hilo alipotembelea shule mbalimabli za Wilaya hiyo na kubaini ukosefu wa vyoo kwa baadhi ya shule na …

Soma Zaidi

Maisha ya watoto Albinism Katumba II Rungwe hatarini

  Maisha ya watoto wenye ulemevu wa ngozi albinism wanaosoma na kuishi kwenye kituo maalum cha walemavu katika shule ya Msingi Katumba 2 wilayani Rungwe mkoani Mbeya yako hatarini kutokana na shule hiyo kukosa mazingira rafiki ya kuishi walemavu hao. Taarifa ya shule hiyo iliyosomwa kwa Naibu Spika wa Bunge …

Soma Zaidi

Wafanyabiashara watakiwa kuondoka Soko la Mwanjelwa

Uongozi wa Jiji la Mbeya umetoa muda wa mwezi mmoja hadi Machi Nne mwaka huu kwa wafanyabiashara wanaozunguka Soko la Mwanjelwa kuhama eneo hilo ili kuwawezesha wafanyabiashara wanaofanya shughuli zao ndani ya soko hilo kuuza bidhaa zao bila bughudha. Hatua hiyo inatokana na malalamiko ya Wafanyabiashara wanaouza bidhaa zao ndani …

Soma Zaidi

Sanje Ligazio achaguliwa kuwa mwenyekiti wilaya ya Kilombero Mkoa wa Morogoro

Kazi ya kuapisha madiwani na uchaguzi wa mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Kilombero iliyokuwa imeahirishwa mara mbili hatimaye imefanyika chini ya uangalizi wa jeshi la Polisi. Katika uchaguzi huo, diwani wa kata ya Sanje Daud Ligazio kutoka chama cha Mapinduzi CCM ametetea nafasi yake na nafasi ya makamu mwenyekiti imechukuliwa na Adamu Sungura diwani …

Soma Zaidi

Viongozi Wakuu waendelea kuwasili jijini Arusha

Viongozi Wakuu wa nchi zinazounda Jumuiya ya Afrika Mashariki wameendelea kuwasili jijini Arusha. Mapema jana Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dokta Ali Mohamed Shein pamoja na Rais Yuweri Museven wa Uganda waliwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro KIA. Tayari mwenyeji wao Rais wa Jamhuri ya …

Soma Zaidi

Kesi ya kugombea maiti Geita yaahirishwa  

  Kesi ya kugombea kuzika mwili wa marehemu Samuel Malugala imeshindwa kusikilizwa baada ya mdaiwa Rahel Washa kutofika mahakamani kwa madai kuwa ni mgonjwa. Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Geita imemuamuru mdaiwa Rahel Washa katika kesi ya kugombea kuzika baina ya waumini wa dini ya kiislamu na familia ya marehemu …

Soma Zaidi

Uongozi  wa machinjio ya Vingunguti walalamikiwa

Wafanyabiashara wa Machinjio ya Vingunguti jijini Dar es salaam wameulalamikia Uongozi wa Chama cha Umoja wa Wafanyabiashara wa Mifugo na Mazao yake Vingunguti (Uwamivi) kuwa chanzo cha mgogoro kwa sababu ya kukiuka makubaliano ya pamoja. Wafanyabiashara hao wamedai kufanya shughuli zao katika mazingira magumu licha ya kuwepo kwa utaratibu mzuri …

Soma Zaidi

Kazi ya ubomoaji jengo la ghorofa 17 yaendelea Dar

Kazi ya ubomoaji Jengo la ghorofa 17 ambalo lilibainika kujengwa chini ya kiwango, imeendelea katikati ya Jiji la Dar es Salaam. Tayari ghorofa tisa kati ya 17 za jengo hilo lililopo katika makutano ya Mtaa wa Indira Gandhi na Barabara ya Morogoro zimebomolewa. Ubomoaji wa jengo hilo ulianza Februari sita …

Soma Zaidi

Polisi Arusha yawaua watuhumiwa wa watatu wa ugaidi

Watu 3 wanaodhaniwa kujihusisha na matukio ya kigaidi wameuwawa usiku wa kuamkia leo katika eneo la sinoni Engosheraton mkoani Arusha baada ya kutokea majibizano ya silaha na Polisi waliofika eneo la tukio kwaajili ya kuwakamata watu hao. Kwa mujibu wa Polisi Mkoani Arusha kati ya watu hao ni mmoja pekee …

Soma Zaidi