AFISA WA FORODHA WILAYANI TARIME AFIKISHWA MAHAKANI.

AFISA WA FORODHA WILAYANI TARIME AFIKISHWA MAHAKANI.

- in Kitaifa

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoani Mara,imemfikisha mahakamani Afisa forodha wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA,kituo cha Sirari EZEKIEL GISUNTE kwa kosa la kudai na kupokea rushwa ya shilingi milioni kumi na tano toka kwa mfanya biashara wa vifaa vya ujenzi aliyekuwa akipitisha bidhaa zake mpakani hapo.

Kamanda wa kikosi cha kuzuia na kupambana na Rushwa mkoani Mara,Holle Makungu ameyasema hayo muda mfupi baada ya afisa huyo kupandishwa na kusomewa mashitaka mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Tarime Mh. Martha Mpanze na kisisitiza kuwa iwapo Gisunte angefanikiwa angeitia hasara serilikali ya shilingi milioni 48.

Mpaka wa Sirari uliopo wilayani Tarime mkoani Mara,umekuwa ukikusanya mapato zaidi ya shilingi bilioni 75.5 kwa mwaka kutokana na malipo ya kodi za bidhaa ziingiazo nchini kupitia mpaka huo.

Kutokana na hali hiyo,taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa mkoani humo,imeweza kubaini na kumfikisha mahakamani afisa forodha wa mamlaka ya mapato katika mpaka huo, Ezekiel Gisunte,kwa tuhuma ya kudai na kupokea rushwa ili kumpunguzia kodi mfanyabiashara wa vifaa vya ujenzi.

Aidha kamanda Holle anasema kuwa Afisa huyo akijua yeye ni mtumishi wa serikali kupitia mamlaka hiyo,alidanganya kwa kutengeneza account nyingine ili asibainike.

Awali mkuu wa wilaya ya Tarime,Grolius Luoga na mkuu wa mamlaka ya mapato mkoani Mara,wakizungumzia tatizo hilo walimtaja Gisunte kwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.

Mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoani Mara kupitia mpaka wa Sirari imedaiwa kupoteza mapato mengi kutokana na watumishi wasio waadilifu.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Wananchi waandamana kukosa maji baada ya mhudumu wa maji kukamatwa na DC

  Na, Ahmed Makongo, Bunda; WANANCHI wa kitongoji