Aliyekuwa rais wa Chad Hissene Habre ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Aliyekuwa rais wa Chad Hissene Habre ahukumiwa kifungo cha maisha jela

- in Habari

hab

Aliyekuwa rais wa Chad Hissene Habre amehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuhusika kwenye uhalifu dhidi ya ubinadamu , ubakaji na utumwa wa ngono.

Hissene Habre alihusika moja kwa moja katika uhalifu huo ambao ulifanyika wakati akiwa rais wa Chad.

Waathiriwa waliokuwa ndani ya mahakama wakati wa kusomwa kwa hukumu hiyo mji Dakar nchini Senegal, walishangilia wakati jaji alimaliza kusoma hukumu.

Bwana Habre anatuhumiwa kwa kuamrisha mauaji ya watu 40,000 wakati wa utawala wake miaka ya 80, madai ambayo ameyakana

Habre alikamatwa nchini Senegal , na kupelekwa uhamishoni mwaka 2013.

 

Source:BBC

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

KESI YA SALUM NJWETE “SCORPION”: Shauri kusomwa Novemba 30 Ilala

Upelelezi wa kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion