Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Emmanuel Minga

Emmanuel Minga

AFISA WA FORODHA WILAYANI TARIME AFIKISHWA MAHAKANI.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoani Mara,imemfikisha mahakamani Afisa forodha wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA,kituo cha Sirari EZEKIEL GISUNTE kwa kosa la kudai na kupokea rushwa ya shilingi milioni kumi na tano toka kwa mfanya biashara wa vifaa vya ujenzi aliyekuwa akipitisha bidhaa zake mpakani hapo. …

Soma Zaidi

TRA YALIA NA WAMACHINGA – DAR

Serikali imeendelea kutekeleza ahadi ya kuwahamisha wamachinga kutoka mitaani na maeneo yasiyoruhusiwa na kwenda katika maeneo maalum ambayo wamepangiwa kwa ajili ya kufanyia biashara zao. Imeelezwa kuwa athari mbalimbali za kuwepo wamachinga wanaofanya biashara kwenye maeneo yasiyoruhusiwa zimeonekana ikiwemo kushuka kwa mapato ya kodi. Vijana wengi, wamejiajiri kupitia biashara hii …

Soma Zaidi

KANDA YA ZIWA YASHINDWA KUKAMILISHA ZOEZI LA MADAWATI

Baadhi ya Mikoa ya Kanda ya ziwa imetajwa kushindwa kumaliza tatizo la madawati kwa shule za msingi na sekondari na kupelekea wanafunzi kuendelea kukaa chini. Mikoa hiyo ni Geita, Mwanza, Mara , Shinyanga na Kigoma ambayo wanafunzi katika shule mbalimbali wanaendelea kukaa chini baada ya agizo la Rais kushindwa kutekelezwa. …

Soma Zaidi

JESHI LA POLISI MKOANI SHINYANGA LAWASHIKILIA BAADHI YA WATU.

Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watu 24 kwa makosa mbalimbali sanjali na watu wengine 2 wanaosadikiwa kuiba gari na kumuua dereva wa gari haina ya Toyota namba T531 aliyetambulika kwa jina la Patrick James aliyeuawa huko mkoani Iringa Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga Muliro Jumanne Muliro amewaambia …

Soma Zaidi

SHULE YA JESHI LA WOKOVU DAR -ES- SALAAM YAPATA MSAADA

Shule ya Msingi Jeshi la Wokovu ya jijini Dar es salaam, inayotoa elimu kwa watoto wenye mahitaji maalum, ina upungufu wa walimu wa Sayansi na Hisabati kwa muda mrefu hivyo imeiomba serikali kuwasaidia watoto wenye uhitaji ili wapate elimu.Hayo yamesemwa wakati wa kupokea msaada wa Baiskeli na Fimbo kwa watoto …

Soma Zaidi

KUBORESHA ZAIDI BANDARI YA TANGA

Mamlaka ya Bandari Tanzania ipo kwenye mchakato wa kupata vifaa vipya vyenye uwezo mkubwa wa kupakia na kupakua shehena na mizigo katika bandari ya Tanga ikiwa ni maandalizi ya kuupokea mradi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Uganda hadi Tanzania. Meneja wa Bandari ya Tanga Henry Arika ametoa kauli hiyo mbele ya …

Soma Zaidi

Wabunge Tanzania wahitaji msaada zaidi

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amekutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka nchi za jumuiya ya Nordic wakiambatana na wawakilishi kutoka shirika la maendeleo la umoja wa mataifa UNDP ambalo limekuwa likiendesha mradi wa kuwajengea uwezo wabunge na watumishi wa Bunge.Katika mazungumzo hayo Spika Ndugai amewaomba wahisani hao …

Soma Zaidi

KESI YA SALUM NJWETE “SCORPION”: Shauri kusomwa Novemba 30 Ilala

Upelelezi wa kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion anayetuhumiwa kumsababishia upofu wa kudumu Saidi Mrisho umekamilika na hatimaye shauri hilo litasomwa Novemba 30 mwaka huu katika mahakama ya manispaa ya Ilala. Njwete anatarajiwa kusomewa mashtaka yake baada ya yale ya kwanza kufutwa ambapo itakuwa ni mara ya kwanza kusikilizwa baada …

Soma Zaidi