Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Joseph Richard (Ukurasa 2)

Joseph Richard

Viongozi CCM watakiwa kutumia rasilimali za chama ili kukuza mapato

Viongozi wa Chama cha Mapinduzi wilayani Magu mkoani Mwanza wametakiwa kutumia rasilimali za chama zilizopo katika maeneo yao kusaidia ukusanyaji wa mapato kwa chama hicho. Ofisi za CCCM wilayani Magu inatajwa kuwa na rasilimali nyingi ambazo zikitumika vyema ukusanyaji wa mapato utasaidia chama kujiendeleza bila kutegemea fedha kutoka ofisi za …

Soma Zaidi

Meneja Mamlaka ya Maji Babati asimamishwa kazi

  Serikali imeingilia kati mgogoro baina ya wananchi na Mamlaka ya Maji Safi na Taka ya mji wa Gallapo GAWASA wilayani Babati mkoani Manyara na kumsimamisha kazi Meneja wa Mamlaka hiyo Mohamed Mstapha. Aidha Serikali imezuia mchakato wa kuunda bodi mpya ya GAWASA uliokuwa ukisimamiwa na meneja huyo na kuwataka …

Soma Zaidi

Rais Magufuli awahimizwa watanzania kudumisha ushirikiano

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli amewataka watanzania kutambua kuwa nguzo kubwa ya mshikamano upendo na ushirikiano ndio itakayoisongesha nchi ya Tanzania kwa kuwa na umoja bila kubaguana kwa namna yoyote ile. Akizungumza katika Ibada ya Jumapili ya pili ya Pasaka katika kanisa la Bikira Maria Parokia …

Soma Zaidi

Viongozi wanaotumia vibaya rasilimali za nchi wanyooshewa kidole

Tanzania inapaswa kuwa na misingi imara ya kizalendo inayolenga kuwabana viongozi wanaobainika kutumia raslimali za taifa kwa manufaa yao wenyewe huku watanzania waliowengi wakibaki katika dimbwi la umasikini. Askofu wa Jimbo katoliki Same Rogath Kimaryo ameyasema maneno hayo wakati akizungumza katika ibada Maalumu iliyoenda sanjari na maadhimisho ya miaka kumi ya Shule ya Sekondari Bendel Memorial …

Soma Zaidi

Wabunge waahidi kutumia Sheria ya bajeti ya 2015 kwa uadilifu

Baadhi ya Wenyeviti na Makamu wa Kamati za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamesema watatekeleza majukumu yao kikamilifu kwa kutumia sheria ya bajeti ya 2015 ili kuondoa migongano isiyo ya lazima na watendaji wa serikali kwenye zoezi la uidhinishaji wa bajeti. Wabunge hao wamesema sheria hiyo bado mpya …

Soma Zaidi

Waziri Kitwanga asema mitandao saba ya wahalifu yabainika Mwanza

Serikali imesema imebaini mitandao saba mkoani Mwanza ya watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu vikiwemo vya ujambazi na wizi wa fedha za miamala kupitia simu za mkononi na kuliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka wote wanaojihusisha na mtandao huo. Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi Charles Kitwanga ametoa kauli hiyo …

Soma Zaidi

Ndege yaangukia gari na kuua

Mtu mmoja ameuawa baada ya ndege kuangukia gari alililokuwa kwenye barabara kuu ya California Marekani. Walioshuhudia tukio hilo wamesema kuwa ndege hiyo ilionekana kama iliyokuwa na matatizo ya injini na ikalazimika kutua kwa dharura kwenye barabara ya Interstate 15 freeway California. Rubani wa ndege hiyo Dennis Hogge hata hivyo alishindwa …

Soma Zaidi

Bunge la Afrika Kusini kujadili hoja ya kumng’oa Jacob Zuma

Bunge la Afrika kusini litajadili hoja ya kumng’oa rais Jacob Zuma madarakani siku ya Jumanne. Spika wa bunge la Afrika Kusini ametoa taarifa hiyo baada ya shinikizo kutoka kwa vyama vya upinzani vikiongozwa na kile cha Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema. Spika Baleka Mbete, amesema wakati umewadia …

Soma Zaidi

Serikali ya Uingereza kuwachunguza wachezaji EPL

Serikali ya Uingereza imeanzisha uchunguzi wa dharura kufuatia tetesi  za wachezaji nyota wa kandanda nchini Uingereza kutumia madawa yaliyopigwa marufuku ya kuongeza nguvu mwilini. Gazeti la Sunday Times limechapisha ripoti ya uchunguzi iliyothibitisha kuwa sio tu wasakataji dimba bali hata waendesha baiskeli, wachezaji Kriketi na hata wachezaji wa tenisi wamekuwa …

Soma Zaidi