Tuesday , October 17 2017
Mwanzo / Joseph Richard (Ukurasa 5)

Joseph Richard

Askari Polisi abainika kutumia vyeti vya kugushi

Zoezi la kuhakiki watumishi hewa lililoamriwa na Rais John Magufuli limemkumba Askari Polisi aliyeajiriwa mwaka 2003 baada ya kubainika kuwa ametumia vyeti vya kugushi. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Zuberi Mwombeji amemtaja Askari huyo kuwa ni Emanuel Nikolas Nyangoli mwenye namba F5425 Pc ambaye baada ya kutuhumiwa kuwa na …

Soma Zaidi

Wanawake 6  kati ya 10 huathirika na tatizo la Endometriosis:

Naibu Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake Wazee na Watoto Dokta Hamis Kigwangala ametoa tathmini ya idadi ya wagonjwa wa Endometriosis ambao huwapata wanawake baada  seli zinazotakiwa kuwa ndani ya mji wa mimba kutunga nje ya eneo hilo. Kigwangala amesema hayo katika Semina ya Endometriosis is real iliyoandaliwa …

Soma Zaidi

Raia wa Japan ajinyonga ofisini

Raia wa Japan amekutwa amejinyonga katika ofisi za kampuni ya Konoike inayojihusisha na uchimbaji wa Visima vijijini Mkoani Tabora unaofadhiliwa na shirika la JAICA. Raia huyo aliyejulikana kwa jina la Akihira Takahashi alikuwa akifanya kazi katika kampuni hiyo katika kitengo cha ufatafiti grade one ya uchimbaji wa Visima Virefu alikutwa amejinyonga katika chumba …

Soma Zaidi

Mkuu wa Shule na Makamu watiwa mbaroni Mwanza  

  Mkuu wa shule ya sekondari Buswelu jijini Mwanza pamoja na makamu wake wanashikiliwa na polisi kwa maagizo ya mkuu wa mkoa wa Mwanza baada ya kukutwa na mihuri 29 ya taasisi mbalimbali za shule kinyume cha sheria.  Kufuatia hatua hiyo mkuu wa mkoa wa Mwanza Magesa Mlongo amemwagiza katibu …

Soma Zaidi

Hofu ya Freemason yatoweka kwa wakazi wa Manyara

Hofu waliyokuwa nayo baadhi ya wakazi wa mkoa wa Manyara kuwa fedha zinazotolewa na mradi wa TASAF awamu wa tatu kwa kaya maskini ni za Freemason imetoweka baada ya jamii kubaini kuwa fedha hizo hazina uhusiano wowote na chama hicho cha siri. Awali wakati Serikali imetangaza kutoa ruzuka ya fedha …

Soma Zaidi

Rais Magufuli ashiriki mazishi ya kifo cha  Selemani Mrisho Kikwete:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Pombe Magufuli ameshiriki mazishi ya Marehemu Selemani Mrisho Kikwete ambaye ni Kaka wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dokta Jakaya Mrisho Kikwete yaliyofanyika katika makaburi ya familia yaliyopo kwenye kijiji cha Msoga wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Mzee Selemani Mrisho Kikwete …

Soma Zaidi

Serikali yaanza kurekebisha sheria kandamizi

Serikali imeanza kuzifanyia marekebisho sheria kandamizi zilizopitwa na wakati ili kuhakikisha wanawake na wasichana wanapatiwa haki zao za msingi inapobainika kuwa wamefanyiwa vitendo vya ukatili. Sheria zinazofanyiwa marekebisho ni ile ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998, sheria ya ardhi namba 4 na sheria ya vijiji namba 5 ya mwaka …

Soma Zaidi