Bei ya nafaka yapanda Mbeya.

Bei ya nafaka yapanda Mbeya.

- in Biashara na Uchumi, Kilimo, Mbeya

BEI ya mazao aina ya nafaka katika baadhi ya masoko jijini Mbeya imepanda ikilinganishwa na bei za mazao hayo katika kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Nafaka zilizopanda bei ni pamoja na zile zinazo Ltumiwa na wananchi walio wengi katika maisha ya kila siku yakiwemo Maharagwe, Mahindi na Mchele ambazo kwa mujibu wa wafanyabiashara, bidhaa hizo kwa sasa zinapatikana kwa taabu kutoka kwa wakulima nafaka nyingine zilizopanda bei ni pamoja na ngano, mtama, ufuta, ulezi na Karanga

Hata hivyo katika Masoko la Soweto na SIDO wafanyabiashara wana amini ongezeko hilo la bei limesabishwa na ukame ambapo wakulima wengi wameficha mavuno yao kwa ajili ya akiba ya chakula kama serikali ilivyo elekeza huku wengine wakiamini ukame ukiendelea bei ya mazao itapanda maradufu na watayauza kwa faida kubwa.
Licha ya changamoto hizo, wafanyabiashara wamesema hali hiyo haijaiathiri kwa kiasi kikubwa biashara hiyo kwa kuwa wateja wanapatikana japo si kwa wingi huku wateja wakidai hakuna namna.

Afrael Manase ni Mchumi wa Halmashauri ya jiji la Mbeya , yeye amesema ongezeko la bei ya nafaka na mazao mengine katika kipindi hiki ni jambo la kawaida tofauti na mwezi Juni mpaka Agosti wakati wa mavuno hivyo amewatoa hofu juu ya kutokea kwa tatizo la njaa.

Imeandikwa na Amina Said, Mbeya

Picha: Mtandao.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Majaliwa: Viwanda havitasimama kwasababu ya migogoro

SERIKALI imesema kuwa haita kubali kuendelea kusimamisha viwanda