Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / CCM Dar yawataka wabunge wake kuelimisha wananchi

CCM Dar yawataka wabunge wake kuelimisha wananchi

Na Grace Semfuko,

Dar es Salaam.

 

Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam kimewataka wabunge wa Mkoa huo kupitia CCM kutoa elimu kwa wakazi wake kuhusiana na masuala ya kijamii yaliyomo kwenye Katiba inayopendekezwa ili wakazi hao waweze kuipigia kura bila kuwa na kikwazo chochote.

 

Katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Dar Es Salaam wajumbe wake wamesema hatua hiyo itawawezesha wakazi wengi kuipigia kura Katiba hiyo ili hatimaye iweze kupita na kutumika kama Katiba mama ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

 

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhan Madabida amesema sambamba na Katiba pia kuna umuhimu wa wananchi kuelimishwa ili waweze kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura.

 

Aidha chama hicho kimesema vikwazo vinavyojitokeza vya wananchi kutoona umuhimu wa Katiba mpya vinatokana na uelewa duni.

 

Pia Madabida amesema zoezi la kampeni ya kuipitisha Katiba hiyo limekaribia akiwataka wanachama wa mkoa huo kuifanyia kampeni Katiba hiyo.

 

Pamoja na mambo mengine kikao hicho pia kinajadili namna ya kushinda kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu.

Kuhusu admin

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *