Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Kimataifa / Chanjo mpya ya HIV yatoa mafanikio

Chanjo mpya ya HIV yatoa mafanikio

Mbinu mpya ya chanjo imeonekana kuwakinga nyani dhidi ya virusi vya HIV ,ripoti ya wanasayansi wa Marekani imesema.

Chanjo kwa kawaida huifundisha kinga ya mwili wa mtu kukabiliana na maambukizi.

Lakini,watafiti katika taasisi ya Scripps mjini Carlifornia wamebadilisha DNA ya nyani hao ili kuzipa seli zao uwezo wa kukabiliana na virusi vya HIV.

Kikosi hicho cha wanasayansi kimetaja hatua hiyo kama mafanikio makubwa na sasa kinataka kuanzisha mbinu hiyo miongoni mwa binaadamu.

chanjo

Majaribio yaliofanywa miongoni mwa nyani hao katika ripoti ya jarida la asili,yalionyesha kuwa nyani walikingwa kutokana aina yoyote ya virusi vya HIV kwa kipindi cha wiki 34.

Watafiti wanaamini kuwa mpango huo huenda ukawa muhimu miongoni mwa watu ambao wana virusi vya HIV.

Mtanfiti bingwa Professa Micheal Farza ameiambia BBC :” tunakaribia kupata tiba ,lakini bado tunakabiliwa na vikwazo hususan katika salama wa kuwapa watu wengi zaidi.

chanjo

Chanjo za HIV zimeshindwa kufanikiwa kwa kuwa virusi hivyo hujibadilisha mara kwa mara kila vinapolengwa na dawa.

Lakini Chanjo hii mpya hulenga eneo ambalo vurusi hivyo hujibadilisha.

BBC

Kuhusu admin

Check Also

Wimbi la Maandamano nchini Marekani

Wimbi la maandamano limepamba moto katika miji mbalimbali ya nchini Marekani wakimtolea ujumbe Rais mteule …

Obama awataka wakuu wa Republican wajitenge na Trump

  Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito kwa viongozi wakuu wa chama cha Republican …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *