Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / DAWASCO KUANZA KUBORESHA MIUNDO MBINU YA MAJI SAFI JIJINI DAR ES SALAAM

DAWASCO KUANZA KUBORESHA MIUNDO MBINU YA MAJI SAFI JIJINI DAR ES SALAAM

04

Shirika la majisafi na majitaka jijini Dar es salaam DAWASCO linaendelea na zoezi la kurekebisha mabomba yote yaliyokuwa yakivujisha maji katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam.

kaimu mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji wa shirika hilo Injinia Aron Joseph amesema hatua hiyo ya Dawasco ilalenga kukausha maeneo yenye madimbwi ya maji yanayotokana na kupasuka kwa mabomba ya maji na kuokoa upotevu wa maji.

Injinia Aron Joseph amesema, zoezi hilo la kurekebisha na kubadilisha mabomba yaliyochakaa katika maeneo 10 ya mikocheni, Masaki na Mwananyamala ili kuokoa maji yanayovuja kabla ya kuwafikia wateja.

Naye mkuu wa Mkoa wa Kinondoni wa Dawasco Bi Judith Hope
Singinika amewataka wakazi wa Kionondoni ambao awajaunganishiwa maji kufika katika ofisi za DAWASCO ili kuunganishiwa maji kwa bei nafuu.

Kuhusu Emmanuel Minga

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *