Halmashauri Iringa yapitisha makadirio ya bajeti, bilioni 59

Halmashauri Iringa yapitisha makadirio ya bajeti, bilioni 59

- in Iringa

Zaidi ya shilingi Bilioni 59.5 zimepitishwa kama mapendekezo ya makusanyo,  katika bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kwa mwaka 2017/ 2018 fedha zitakazosaidia katika uendeshaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo.

 Rasimu hiyo ya mpango wa bajeti ambayo pia imelega kutumia kiasi hicho cha shilingi Bilioni 59.5, fedha zitakazotokana na makusanyo katika vyanzo mbalimbali vya mapato.

Mapendekezo ya fedha hizo kwa asilimia kubwa yanaelezwa kuwa yatapelekwa katika mishahara ya watumishi, ambapo ruzuku ya serikali kuu inatajwa kuwa ni zaidi ya shilingi Bilioni 47,  huku michango mbalimbali ya wananchi katika miradi ya maendeleo – ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni nane.

Asilimia kubwa ya fedha hizo zinatajwa kuelekezwa katika ulipajio wa mishahara na uendeshaji wa Halmashauri kwa mujibu Deonis Sui Mtunza Hazina wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Abel Mgimwa ni Afisa Mipango wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, anaona matumizi makubwa ya makusanyo ya fedha yanahudumia uendeshaji wa Halmashauri kuliko ujenzi wa miradi ya maendeleo.

 Imeandikwa na Oliver Motto, Iringa – Star TV

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Waziri Mkuu Majaliwa atua Iringa tayari kwenda Njombe.

​Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa ametua leo asubuhi