Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Biashara na Uchumi / Halmashauri kuwabana mama lishe kuanza kutumia mashine za EFD

Halmashauri kuwabana mama lishe kuanza kutumia mashine za EFD

efd

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Moshi, wamepitisha azimio la kuwabana kutumia mashine za kielekroniki (EFD), mama lishe na watoa huduma ya vinywaji wanaopewa zabuni ya kuhudumia vikao vya watumishi wa halmashauri hiyo.

Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Peter Minja, aliyasema hayo jana baada ya kukabidhiwa hati safi na Mwakilishi wa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ya mwaka wa fedha 2015/16.

“Ili kuchangia fedha za serikali, watoa huduma wote wanaopata zabuni za halmashauri, lazima watumie mashine za EFD. Wamepewa muda wa mwezi mmoja wawe na mashine hizo ili kuongeza makusanyo ya halmashauri,”alisema Naibu Meya huyo

Alisema Baraza la Madiwani limepokea kwa mikono miwili maoni na maelekezo ya CAG ya kuwataka kuboresha ukusanyaji wa mapato ya halmashauri hiyo kutumia mashine za EFD.

Kwa mujibu wa Minja halmashauri hiyo imefanikiwa kuongeza makusanyo yake ya kodi hadi kufikia shilingi Bilioni 6 kwa mwaka, huku ikipata hati safi kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo.

Akizungumzia changamoto ya Manispaa hiyo kupata nafasi ya pili katika usafi na utunzaji wa mazingira kwa mwaka 2015/16, alisema kulikuwapo na ushindani mkubwa ndio maana ikaangukia nafasi hiyo. kikombe.

Alisema ushindi huo unaipa manispaa hiyo chachu ya kuongeza jitihada za usafi na utunzaji wa mazingira katika kata zilizopo pembezeni mwa mji wa Moshi, ikiwa ni pamoja na kuimarisha jitihada za uzoaji wa taka katika maeneo mbali mbali.

Kuhusu Emmanuel Minga

Check Also

KAZI ZA SANAA NCHINI: Utafiti duni wachangia kushusha ubora wake

Katibu mtendaji wa bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso anasema wasanii wa maigizo nchini hawana …

WALIONUNUA VIWANDA MKOANI MARA

Mkuu wa mkoa wa Mara Dokta Charles Mulingwa amewataka wawekezaji waliouziwa viwanda na serikali mkoani …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *