Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Jamii yatakiwa kuwasaidia waliopata mimba za utotoni.

Jamii yatakiwa kuwasaidia waliopata mimba za utotoni.

Na Abdalla Pandu,

Njombe.

Jamii imetakiwa kutowatenga na kuwatelekeza watoto wa kike waliopata ujauzito wakiwa katika umri mdogo na wanafunzi shuleni kwa bali waendelee kuwatunza na kuwatafutia fursa za kuwaendeleza kitaaluma wakiwapa mbinu za kujiepusha na viashiria vinavyoweza kuwatumbukiza tena katika tatizo hilo.

 

Vijana wengi waliotumbukia katika kupata mimba za mapema  kuonekana ni wahuni na hawana mchango katika familia ,hutengwa na kutelekezwa hivyo huwa ni mzigo katika familia na hata Taifa kwa ujumla hasa wasipoendelezwa.

 

Akizungumza na star tv  Wakati wa ziara ya wanafunzi na walimu wa chuo cha Mwenge Community center kutoka Zanzibar waliofika mkoani NJOMBE katika ziara ya mafunzo mwalimu mkuu  wa Chuo  cha Maeneleo ya wananchi  wilaya ya Njombe  GEORGE   OSCAR  anasema  kuwa jamii kwa muda mrefu huwatenga vijana hao na hata wale wanaowapa ujauzito huwakimbia ,Hali ambayo imewasukuma katika chuo hicho kuwaendeleza vijana hao katika fani mbali mbali ili warejeshe matumaini ya kueneleza maisha yao katika jamii.

 

Alisema pamoja na makosa yao bali jamii haina budi  kuwapatia haki zao za msingi baala ya kuwatenga ikiwa ni pamoja na kuwaeneleza kimasomo.

 

Pamoja na mambo mengine Mwalimu Oscar alisema wamekuwa wakiwapokea vija hao na watoto wao chuoni hapo na kuwaendeleza huku akieleza mafanikio makubwa yameanza kupatikana kwa vijana waliohudhuria mafunzo chuoni hapo hapo.

 

Star tv pia ilipata fursa ya  kuzungumza na mmoja kati ya vijana walioathirika na hali hio ambae ameendelezwa katika chuo hicho   SCOLATICA B. NGULO  akizungumza wakati akitowa ushuhua jinsi alivyotengwa mara baaa ya kupata ujauzito  akiwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza, huku akielezea mafanikio alioyapata mara baaa ya kumaliza masomo yake chuoni hapo’

 

Huku akiwasihi wasichana hasa walioopo mashuleni kuwa makini na kujiepusha na masuala ya mapenzi wakati wakiwa mashuleni jamba ambalo linaharibu mustakbali wa masomo yao.

 

 

Kuhusu admin

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *