Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / JESHI LA POLISI MKOANI SHINYANGA LAWASHIKILIA BAADHI YA WATU.

JESHI LA POLISI MKOANI SHINYANGA LAWASHIKILIA BAADHI YA WATU.

Jeshi la polisi mkoani Shinyanga linawashikilia watu 24 kwa makosa mbalimbali sanjali na watu wengine 2 wanaosadikiwa kuiba gari na kumuua dereva wa gari haina ya Toyota namba T531 aliyetambulika kwa jina la Patrick James aliyeuawa huko mkoani Iringa

Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani Shinyanga Muliro Jumanne Muliro amewaambia waandishi wa habari kwamba jeshi lake linaendelea na msako mkali dhidi ya waalifu mkoani Shinyanga

Jeshi la polisi limefanikiwa kupatikana kwa Gari  hilo lililokuwa limeibwa huko Wilayani Mufindi mkoani Iringa sanjali watuhumiwa 2 wanaosadikiwa kuiba gari pamoja na kumuua dereva wa gari hili Patrick James kisha mwili wake kuutupa kando ya mto  Ruaha

Kamanda wa Jeshi la Polisi hapa Mkoani Shinyanga Muliro Jumanne Muliro amesema msako mkali unaoendelea mkoani Shinyanga wa kuwasaka waalifu ndio uliozaa matunda ya kuwakamata watuhumiwa  na gari hili.Kamanda Muliro anatoa wito kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga kutoa taarifa za uhalifu ili ziweze kufanyiwa kazi mapema

Kuhusu Emmanuel Minga

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *