KANDA YA ZIWA YASHINDWA KUKAMILISHA ZOEZI LA MADAWATI

KANDA YA ZIWA YASHINDWA KUKAMILISHA ZOEZI LA MADAWATI

- in Kitaifa

Baadhi ya Mikoa ya Kanda ya ziwa imetajwa kushindwa kumaliza tatizo la madawati kwa shule za msingi na sekondari na kupelekea wanafunzi kuendelea kukaa chini.

Mikoa hiyo ni Geita, Mwanza, Mara , Shinyanga na Kigoma ambayo wanafunzi katika shule mbalimbali wanaendelea kukaa chini baada ya agizo la Rais kushindwa kutekelezwa.

Akipokea msaada wa madawati 3,500 kutoka Benki ya NMB, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene ameipongeza mikoa ambayo imekamilisha zoezi hilo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), George Simbachawene amewataka Wakuu wa Mikoa ambao mikoa yao haijakamilisha agizo la Rais kuhakikisha kila shule ya msingi na sekondari inakuwa na madawati hadi kufikia Januari mwakani.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Wananchi waandamana kukosa maji baada ya mhudumu wa maji kukamatwa na DC

  Na, Ahmed Makongo, Bunda; WANANCHI wa kitongoji