Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Biashara na Uchumi / KAZI ZA SANAA NCHINI: Utafiti duni wachangia kushusha ubora wake

KAZI ZA SANAA NCHINI: Utafiti duni wachangia kushusha ubora wake

Katibu mtendaji wa bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso anasema wasanii wa maigizo nchini hawana budi kujikita zaidi katika kazi zenye viwango na ubora ili kuingia katika soko la ushindani.

Kwa sasa tasnia ya Sanaa ya maigizo imekuwa sehemu ya Ajira kwa vijana wengi lakini bado ina kabiliwa na changamoto ya ubora na hivyo kuwafanya wasanii kuendelea kuganga njaa.

Mpango huu unawakutanisha pamoja zaidi ya wasanii 250 kutoka Wilaya mbali mbali za mkoa wa Mwanza lengo likiwa kuwajengea uwezo wadau wa tasnia ya Filamu.

Mpango huu unaonekana kuwa fursa ghadhimu na mwazo mazuri wa kuleta mabadiliko chanya kwa taifa na wasanii nchini.

Afisa elimu mkoa wa Mwanza Mwalimu Khamis Maulid  akifungua mafunzo haya anawataka washiriki kuzingatia suala la maadili ya Tanzania na kutupia mbali tamaduni za kimagharibi.

Si zaidi ya siku tatu wasanii hawa na viongozi wataketi ukumbini hapa kujifunza mbinu mbali mbali za kuboresha hadhi ya kazi ya Sanaa ikiwemo uandishi wa muswada wa Filamu,utafiti bila ya kusahau wajibu na majukumu ya bodi ya Filamu katika kukuza Sekta hiyo.

Kuhusu Emmanuel Minga

Check Also

WALIONUNUA VIWANDA MKOANI MARA

Mkuu wa mkoa wa Mara Dokta Charles Mulingwa amewataka wawekezaji waliouziwa viwanda na serikali mkoani …

Rais Magufuli acharuka, aagiza bodi ya pamba kuondoka Dar kuhamia mikoa ya kanda ya ziwa.

Rais John Pombe Magufuli ameiagiza Bodi ya Pamba Tanzania (TCB) kuhamia katika mikoa ya Kanda …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *