Kikao cha kwanza cha MUUNGANO 2017 chafanyika Zanzibar

Kikao cha kwanza cha MUUNGANO 2017 chafanyika Zanzibar

- in Kitaifa, Zanzibar

Kikao cha kwanza katika mwaka 2017 cha kamati ya pamoja  ya serikali ya Zanzibar na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  kuhusu masuala ya kero za muungano kimekaa visiwani Zanzibar na kujadili changamoto mbali mbali zilizopo katika muungano huo kwa kipindi kirefu na kupatiwa ufumbuzi baadhi yake.

Kikao hicho kimepitia masuala mbali mbali yaliojadiliwa kikao kilichopita na kuangalia changamoto mpya na mara baada ya kikao hicho cha siku moja waziri wa nchi afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametoaa ufafanuzi jinsi ya makubaliano na namna mjadala ulivyokwenda Mhe. Mohammed Aboud

Pamoja na mambo mengine waziri Aboud amesema kuwa katika baadhi ya changamoto nyengine zilizojadiliwa ni pamoja na kuhusu usajili wa vyombo vya moto na bidhaa zinazozalishwa Zanzibar kuingizwa katika soko la Tanzania Bara.

Kwa upande wake waziri wa nchi afisi ya makamu wa rais Muungano, Mhe. Januari Makamba anasema wamepitia kumbukumbu zote za vikao vilivyopita na kukubaliana  sambamba na ajenda kumi kuwasilishwa.

Kikao hicho ni muendelezo wa vikao vya kujadili changamoto mbali mbali za muungano vyenye lengo la kuimarisha muungano wa Tanzania.

Imeandikwa na Abdalla Pandu.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Wananchi waandamana kukosa maji baada ya mhudumu wa maji kukamatwa na DC

  Na, Ahmed Makongo, Bunda; WANANCHI wa kitongoji