KUBORESHA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE:Serikali yahimiza ujenzi wa mabweni

KUBORESHA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE:Serikali yahimiza ujenzi wa mabweni

- in Kimataifa

Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hasan amehimiza ujenzi wa mabweni ya wasichana katika shule mbalimbali nchini ikiwa ni sehemu ya kuboresha elimu kwa watoto wa kike.Inabainika bado kuna tatizo la wasichana kutomaliza masomo yao kwa kupata mimba za utotoni huku sababu mojawapo ikitajwa kwa kundi hilo kukutana na vikwazo vya kutongozwa na wanaume wakati wakiwa barabarani kuelekea shuleni.

Ni uungwana na taratibu za kitanzania kila anapofika mgeni hukaribishwa kwa nderemo na vifijo.Ziara ya Makamu wa Rais Mkoani mwanza inaendelea, siku akianzia wilayani Misungwi kuweka jiwe la uzinduzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Idetemya.Upatikanaji wa Elimu kwa wasichana bado sio wa kuridhisha huku wakizongwa na kila aina ya vikwazo wanapokuwa njiani kuelekea shuleni.

Suala la ujenzi wa mabweni ya wasichana sasa linaangaliwa kwa jicho la tatu, Makamu wa Rais pia anaweka jiwe la msingi la ujenzi wa bweni katika shule ya Sekondari Archbishop Mayala ya wilayani kwimba.Siku zote Mama ni Mama jambo hili linamuuma na hata kuamua kuchangia mifuko 200 ya saruji na mabati 100 kwa ajili ya kuharakisha ujenzi wa bweni hilo.Makamu wa Rais Mama Samia aidha ametembelea mabwawa ya kufugia samaki unaosimamiwa na vikundi mbalimbali chini ya mradi wa kutunza mazingira ya Ziwa Viktoria (LVEMP) awamu ya pili.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

TAFAKARI YA UTAWALA MPYA U.S.A

Mawaziri  wa mambo  ya  nje  wa Ulaya  wamekutana