Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Michezo na Burudani / Kuimarishwa uwanja wa Nyamagana

Kuimarishwa uwanja wa Nyamagana

Mipango ya kuendeleza soka la vijana huenda ikawa na tija endapo tu serikali chini ya ilani ya Chama cha Mapinduzi itafikia makubaliano ya sera ya kubinafsisha baadhi ya viwanja vyake vya michezo inavyovimiliki nchini.Hatua hiyo inaweza kufikia viwango vya kimataifa vya ubora wa viwanja kwa wadau kujitokeza kuwekeza na kuleta hamasa zaidi kwa vijana katika kujiendeleza kimichezo kuanzia ngazi za chini.

Matumaini mapya yanarejea, mboni za macho ya wanamichezo zinapendezeshwa na taswira mpya  ya uwanja huu wa Nyamagana ulio katikati ya jiji la Mwanza ukijani uliotawala hapa unafufua matumaini ya kuianza hatua ya kuwa na viwanja vyenye hadhi ya kimataifa  hii ni hatua nzuri.

Si haba! uwanja huu umekiamsha Chama tawala cha Mapinduzi (CCM) juu ya viwanja vyake zaidi ya 20 inavyovimiliki nchi kutizama upya sera itakayo toa nafasi kwa wadau kuwekeza na kuviboresha ili kuendeleza  miundombinu ya soka.Huenda michezo ikianzia ngazi za chini kwa miundo mbinu rafiki italeta mchango chanya kwa Taifa.

Kwa upande wa kanda ya ziwa sasa viwanja vilivyorekebishwa kisasa ni viwili ni ule wa Kaitaba kule Kagera na uwanja huu wa Nyamagana hapa mwanza.

 

Kuhusu Emmanuel Minga

Check Also

Arusha wasusia uchaguzi wa viongozi

Chama cha riadha mkoa wa Arusha kimepinga kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa shirikisho la …

• SHERIA 17 ZA SOKA: Waamuzi walaumiwa kuziweka

Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara, ikifikia tamati ya mzunguko wa kwanza, mashabiki wa soka wametoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *