Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Lowasa ampongeza Rais Magufuli kwa utendaji wake

Lowasa ampongeza Rais Magufuli kwa utendaji wake

lowassa copy

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa amempongeza Rais John Magufuli kwa utendaji wake tangu ashike nafasi ya urais Novemba mwaka jana.

Hata hivyo, Waziri Mkuu huyo wa zamani amebainisha kuwa ingekuwa ni yeye amepata nafasi ya urais, angeanza na vipaumbele vyake ambavyo ni ajira na maslahi ya walimu ili kuboresha zaidi maeneo hayo.

Lowassa aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akihojiwa na mtangazaji Tido Mhando kwenye kipindi cha Funguka, kinachorushwa na Televisheni ya Azam.

Alikiri kuwa Dk Magufuli hadi sasa ameonekana kufanya vizuri katika utendaji wake, ikiwemo suala la ufisadi na hatua yake ya kutekeleza kwa vitendo kuhamishia serikali mkoani Dodoma.

“Amefanya kazi nzuri katika maeneo fulani, amefanya vizuri sana. Kuna maeneo amesema mwalimu unaweza kufagia shilingi, na yeye amefagia shilingi. Ila kuuna maeneo kwa maoni yangu ningeyapa kipaumbele zaidi kwa mfano ajira,” alisisitiza.

Alisema suala la ajira bado Serikali ya Awamu ya Tano, haijalipa msukumo wa kutosha kwani Watanzania wengi bado wanataabika na ukosefu wa ajira.

“Hawa mama ntilie, bodaboda na wahitimu wengi wa vyuo vikuu hatuwatazami,” alisema Lowassa aliyeshindwa na Dk Magufuli katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana.

Alisema hata katika kampeni za Uchaguzi Mkuu zinazoendelea nchini Marekani, Rais Barack Obama wakati akihutubia wananchi, alibainisha wazi kuwa kipindi chake cha uongozi amefanikiwa kutengeneza ajira zaidi ya milioni 1.5.

Katika elimu, waziri mkuu huyo wa zamani pamoja na kupongeza hatua ya Magufuli ya kuanzisha operesheni madawati, lakini alibainisha wazi kipaumbele chake kingekuwa katika kuboresha zaidi madarasa na maslahi ya walimu.

Alisema anajivunia kuwa sehemu ya uanzishwaji wa shule za kata nchini, ambazo kwa sasa pamoja na kuanza na changamoto, lakini zimeanza kufanya vizuri na baadhi yake zimeshika nafasi za juu katika mitihani ya kidato cha nne.

Hata hivyo, Serikali ya Awamu ya Tano katika bajeti yake ya kwanza ya 2016/17 imekuwa na mpango kabambe wa mapinduzi ya viwanda kwa kuhakikisha idadi ya viwanda inaongezeka nchini, ikiwemo kufufua viwanda vyote vilivyokufa, lengo likiwa ni kuwa na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025, lakini pia kuongeza ajira. Aidha, katika suala la maslahi ya walimu, tayari Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alibainisha kuwa azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha inawawekea mazingira mazuri walimu ikiwemo kuongezea mishahara pamoja na vitendea kazi vya kufundishia. Hivi karibuni, Rais Magufuli alitangaza wazi kuwa baada ya kupata mafanikio katika operesheni ya utengenezaji wa madawati nchi nzima, wadau wa maendeleo watumie nguvu na kasi waliyoanza katika madawati, kujenga madarasa ili kupunguza tatizo la upungufu wa madarasa. “Nimeanza na madawati kwa kuwa naamini ni muhimu kwa mwanafunzi kwani, mwanafunzi anaweza kuendelea kusoma akiwa na dawati na ubao hata chini ya mti kuliko kukaa chini. Haya si mazingira mazuri ya kusomea,” alisema Magufuli. Kuhusu serikali kuhamia Dodoma, Lowassa alisema suala hilo kila rais wa Tanzania aliyepita akianzia Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi, William Mkapa na Jakaya Kikwete, alikuwa na dhamira ya

Kuhusu Emmanuel Minga

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *