Maafisa wanne Kigoma wasimamishwa kazi kwa tuhuma za udanganyifu

Maafisa wanne Kigoma wasimamishwa kazi kwa tuhuma za udanganyifu

- in Habari

Kigoma_kituo_cha_reli_2012_Tamino

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia General Mstaafu Emmnuel Maganga ameagiza kusimamishwa kazi kwa Maafisa maendeleo wanne  wa  Halmashauri za Manispaa ya Kigoma Ujiji na Wilaya ya Kigoma kwa tuhuma za uzembe na udanganyifu kwa kuweka miradi hewa katika ukaguzi wa mbio za mwenge.

Aidha mkuu huyo wa mkoa ameziagiza Mamlaka husika  kuwasimamisha kazi  makaimu wakurungezi wa halmashauri hizo Sultani Ndoliwa aliyekuwa akikaimu nafasi ya mkurugenzi Manispa ya Kigoma ujiji  na  Dokta  Revocatus Masanja aliyekuwa kaimu   mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kigoma ili kupisha uchunguzi.

Mwenge wa uhuru unaendelea na mbio  zake mkoa kigoma ambapo unatarajiwa kuhitimishwa  mbio zake mkoani hapa  julay  23  na kubidhiwa mkoa wa kagera.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

KESI YA SALUM NJWETE “SCORPION”: Shauri kusomwa Novemba 30 Ilala

Upelelezi wa kesi inayomkabili Salum Njwete maarufu kama Scorpion