Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Madhehebu ya dini yapaswa kuungwa mkono

Madhehebu ya dini yapaswa kuungwa mkono

 

Baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Bunda mkoani Mara, wamesema kutokana na madhehebu ya dini kuwa na mchango wa maendeleo ya jamii katika Nyanja mbalimbali yanapaswa kuungwa mkono na wananchi wote.

Katika harambee ya kuchangia ujenzi wa chuo cha ufundi stadi (VETA), kitakachoengwa na Kanisa la Waadventista Wasabato la Bomani ndipo wananchi hao wanapaza sauti zao.

 Wamesema kuwa madhehebu ya dini ni wadau wakubwa wa Serikali katika suala zima la maendeleo, hususani katika sekta za afya na elimu, ambapo yamekuwa yakitoa mchango mkubwa kwa kutoa huduma mbalimbali zinazogusa wananchi.

Wamesema kuwa vijana wengi wamekuwa wakimaliza elimu ya msingi na hata sekondari na kukosa ajira na kwamba iwapo chuo hicho cha Veta kikikamilika, vijana watapata fursa ya kujiunga nacho, na kupata elimu ya ufundi stadi, itakayowawezesha kuajiriwa na taasisi za watu binafsi, au serikali ama kujiajiri wao wenyewe.

 Mkuu wa Wilaya ya Bunda aliyekuwa mgeni rasmi katika harambee hiyo, Joshua Mirumbe, amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa madhehebu ya dini na kuongeza kuwa Kanisa limepewa majukumu mengi sana, ikiwa ni pamoja na kuhubiri mambo ya afya na kutoa elimu kwa jamii ili waweze kupata maarifa.

Mirumbe amewataka wananchi wilayani humo kuliunga mkono Kanisa hilo na kuwekeza kwa kuchangia kwenye elimu, badala ya fedha zao kuchangia  mambo ya starehe.

Aidha, amesema kuwa kuhusu mpango wa Serikali kutoa elimu bure kwa wananfunzi tayari Wilaya hiyo imeshapokea shilingi milioni 106.

 Akisoma taarifa ta Kanisa hilo kuhusu mapango wake wa kujenga chuo cha Veta, Gerald Rubairo, amesema kuwa tayari wameshapata eneo la ekari 17, kwa ajili ya ujenzi wa chuo hicho na kituo cha afya, ambapo pia katibu wa Kanisa hilo jimbo la Musoma  Enock Sando, amesema kuwa maendeleo makubwa katika sehemu mbalimbali hapa ulimwunguni, yanatokana na nchi pamoja na taasisi mbalimbali kuwekeza kwenye elimu ya ufundi.

Katika harambee hiyo, iliyoendeshwa na mkuu wa Wilaya ya Bunda, Joshua Mirumbe, zaidi ya shilingi milioni 12.7 zimepatikana zikiwemo ahadi na pesa taslimu.

 

Kuhusu Joseph Richard

Check Also

Watu wanne washikiliwa Morogoro kwa jaribio la kuvamia kituo cha polisi

Polisi mkoani Morogoro inawashikiria watu wanne wakazi wa Mzumbe wilayani Mvomero, kwa tuhuma za kujaribu …

Maafisa wanne Kigoma wasimamishwa kazi kwa tuhuma za udanganyifu

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia General Mstaafu Emmnuel Maganga ameagiza kusimamishwa kazi kwa Maafisa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *