Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amezuia uvamizi na shughuli za ujenzi katika shamba lililopo Mtaa wa Nondo, Kijiji cha Mabwepande – Mtakuja Jijini Dar Es Salaam hadi pale uchunguzi zaidi ukakapokamilika.

Shamba hilo ambalo kwasasa linamilikiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye, lilivamiwa na Wananchi kwa madai kuwa lilikuwa halitumiki kwa  shughuli za Maendeleo wala Makazi.

 Ni katika ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye na wananchi katika eneo la mabwepande iliyokuwa na lengo la  kutafuta suluhisho la mgogoro wa Ardhi kati ya wananchi na Sumaye.

Waziri Mstaafu Sumaye amedai kuwa shamba hilo ni lake na kwamba anavyo vielelezo vyote vya umiliki halali sambamba na kuendelea kulipia kodi ya ardhi.

 Baadhi wa wananchi katika eneo hilo wamesema waliamua kutumia eneo hilo kutokana na kuona halitumiki na limekaaa kama shamba pori.

 Baada ya Mazungumzo yaliyodumu kwa zaidi ya saa tatu, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ametoa wiki za kufanyika kwa uchunguzi ili kuweza kujua mmiliki halali wa eneo hilo.

 Wilaya ya Kinondoni ni miongoni mwa wilaya ambazo zimekuwa zikikabiliwa na changamoto ya migogoro ya Ardhi kutokana na kuwepo kwa migongano ya mara kwa mara ya uhalali wa umiliki.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here