Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kimataifa / Marekani yaitupia lawama Urusi, shambulio la Syria

Marekani yaitupia lawama Urusi, shambulio la Syria

sirip

Marekani imesema ndege za kivita za Urusi zilihusika kushambulia msafara wa misaada nchini Syria siku ya Jumatatu na kusababisha vifo.

Maafisa wa Marekani wameiambia BBC ndege mbili za kivita za Urusi aina ya SU-24, zilikuwa angani, sambamba na msafara huo wa magari, wakati tukio hilo likitokea.

Hata hivyo Urusi imekana na kusema kuwa ndege hizo hazikuwa zake wala za Syria, na kutupia lawama wapiganaji wa waasi.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ndege zake zinazojiendesha zenyewe zilikuwa zikifuatilia msafara huo, lakini kamera zao zilijizima kabla ya mashambulizi kuanza.

Shambulio hilo la Jumatatu lilifanyika saa kadhaa baada ya serikali ya Syria kutangaza kumaliza wiki ya kusitisha mapigano.

#BBC

Kuhusu Emmanuel Minga

Check Also

Wimbi la Maandamano nchini Marekani

Wimbi la maandamano limepamba moto katika miji mbalimbali ya nchini Marekani wakimtolea ujumbe Rais mteule …

Obama awataka wakuu wa Republican wajitenge na Trump

  Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito kwa viongozi wakuu wa chama cha Republican …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *