Kutohusishwa kwa madiwani katika sheria ya manunuzi ya Umma kumetajwa kuwa miongoni mwa mianya ya matumizi mabaya ya fedha zinazopelekwa kwa ajili ya miradi ya jamii.Kwa mujibu wa sheria ya manunuzi ya mwaka 2001, madiwani wanapaswa kuwa wasimamizi tu wa hatua zote lakini watendaji wamekuwa wakitumia vibaya nafasi hiyo na kusababisha upotevu wa rasilimali fedha.

Matumizi mabaya ya fedha za umma yameendelea kuzikumba halmashauri za Wilaya, Miji na majiji hapa nchini yakiacha makovu kwa ustawi wa jamii huku yakiboresha uchumi wa watu binafsi.Kwa miaka miwili ya fedha iliyopita, Jiji la Mwanza limepata hati yenye mashaka mfululizo, kitendo kinachoashiria kukiukwa kwa kanuni za manunuzi ya umma.Madiwani wanaona kutengwa kwao katika sheria kunachangia utekelezaji mbovu wa manunuzi na kuongeza kadhia kwa jamii kupitia miradi mibovu.

Mradi wa kukuza ushiriki wa wananchi katika matumizi ya raslimali za umma chini ya taasisi ya BED Mkoani Mwanza unachukuwa jukumu la kuwaelimisha madiwani wa jiji la mwanza majukumu yao ya kulinda, kusimsmia na kuwajibisha utendaji mbovu  ili kuokoa upotevu wa raslimali.

Matarajio ya wadau hawa sasa ni kufanyika kwa uchambuzi wa matumizi ya fedha za umma katika kata mbalimbali za jiji la mwanza ili kujenga misingi imara ya kiusimamizi dhidi ya raslimali za umma.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here