Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Biashara na Uchumi / Mbegu bora za mpunga, Upatikanaji wake changamoto Tanzania

Mbegu bora za mpunga, Upatikanaji wake changamoto Tanzania

Na Kasilda Mgeni Mulimila,

Mvomero.

Tanzania inakabiliwa na tatizo la upatikanaji wa mbegu bora za Mpunga licha ya uzalishaji wa zao hilo kuongezeka kutoka hekta 490,000 mwaka 1998 hadi kufikia hekta 854,000 mwaka 2011.

Miongoni mwa sababu ya ukosefu huo ni kutokuwepo kwa wataalamu  wa kutosha wenye uzoefu wa kuzalisha mbegu bora za Mpunga zenye viwango vinavyotakiwa.

Sababu zingine ni ukosefu wa mitaji na motisha  kwa makampuni  ya mbegu ya kizalendo kuwekeza katika miundo mbinu  ya  kuzalisha na kusindika mbegu hizo na kuzisambaza  kwa wakulima kwa wakati mwafaka pamoja na wakulima kukosa elimu ya mbegu bora na mwamko mdogo  wa matumizi ya mbegu hizo.

Ni katika maonesho ya uzalishaji mbegu bora mpya  ya Mpunga aina ya TXD 306  SARO 5  yanayofanyika  kwenye mashamba ya ushirika wa WAWAKUDA  Wami Dakawa wilayani Mvomero  ambayo imezalishwa na kampuni ya mbegu ya  TANSEED Internatinal yenye makao yake makuu mjini morogoro kwa kushirikiana na mradi wa nafaka nchini.

Mkurugenzi  TANSEED International Isaka  Mashauri na Hezlon Tusekelege Mtafiti Kituo cha utafiti wa Mbegu Dakawa wameeleza kuwa nchi inavyokabiliwa na upungufu mkubwa wa mbegu bora za zao la Mpunga.

Wamesema mbegu hiyo  mpya itakuwa muarobaini wa tatizo hilo nchini.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera aliyekuwa mgeni rasmi katika maonesho hayo ya mbegu bora ya SARO 5 amepata fursa ya kutembelea shamba bora la mfano la mkulima aliyetumia mbegu hiyo mpya.

Akihutubia wananchi Bendera ametoa onyo kali dhidi ya mawakala wa mbegu nchini wasio waaminifu wanaowadanganya wakulima na kuwauzia mbegu feki kuwa serikali iko macho na itawachulia hatua kali watakaobainika.

Mbegu bora ya SARO 5 imeelezwa kuwa na sifa ya kutoa mavumo  kati ya magunia 30 hadi 40 kwa ekari, hukomaa mapema kati ya miezi 3 hadi 4, punje zake ni nyembamba na ndefu  na inanukia vizuri na hivyo kuwa kivutio katika soko  kutokana na kuanza kupendwa na walaji wengi.

Kuhusu admin

Check Also

KAZI ZA SANAA NCHINI: Utafiti duni wachangia kushusha ubora wake

Katibu mtendaji wa bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisso anasema wasanii wa maigizo nchini hawana …

WALIONUNUA VIWANDA MKOANI MARA

Mkuu wa mkoa wa Mara Dokta Charles Mulingwa amewataka wawekezaji waliouziwa viwanda na serikali mkoani …

Maoni

  1. Napenda kujua iyo mbegu ya mpunga SARO 5 inapatikana wapi.?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *