Mbunge Njalu kuchangia madawati 5,000

 Mbunge Njalu kuchangia madawati 5,000

- in Kitaifa

Mbunge wa jimbo la Itilima mkoani Simiyu Njalu Silanga ameahidi kutengeneza madawati elfu tano yenye thamani ya milioni 400 ili kukabiliana na changamoto ya uhaba wa madawati wilayani Itilima

Hii ni sehemu ya mkakati wa kuunga mkono agizo la Rais Magufuli katika kumaliza changamoto ya uhaba wa madawati nchini.

Njalu amesema yeye akiwa mdau wa elimu ameamua kuchangia madawati hayo ili kuleta chachu ya kusoma watoto ambao baadhi yao wamekuwa wakikata tamaa ya kuendelea na masomo kwa kukaa sakafuni,

Baadhi ya wadau wa maendeleo wamempongeza mbunge huyo kwa msaada huo mkubwa ambao utasaidia kupunguza changamoto ya madawati inayoikabili wilaya ya itilima na pia kupunguza utoro mashuleni

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony Mtaka amewataka wana Itilima kuuimarisha mfuko wa elimu ambao utasaidia kuongeza kiwango cha ufaulu na pia utasaidia ujenzi wa mabweni na nyumba za walimu.

Wilaya ya Itilima inakabiliwa na upungufu wa madawati 16,000

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Wananchi waandamana kukosa maji baada ya mhudumu wa maji kukamatwa na DC

  Na, Ahmed Makongo, Bunda; WANANCHI wa kitongoji