Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Migogoro ya wakulima na wafugaji. 3 wapoteza maisha, wananchi waomba msaada wa serikali.

Migogoro ya wakulima na wafugaji. 3 wapoteza maisha, wananchi waomba msaada wa serikali.

Wananchi wa Vijiji vya Kiwanda na  Kilongo-Samanga  wanaoishi Mpakani mwa Tanzania na Kenya katika Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, wameziomba Serikali za Tanzania na Kenya kuingilia Kati Mgogoro wa Wakulima na Wafugaji kabla haujaleta madhara makubwa.Ombi hilo limekuja siku chache baada ya wakulima watu wa Kijiji cha Kiwanda Wilayani humo  kupigwa na kujeruhiwa vibaya  kichwani na Mikononi na Wafugaji wa Jamii ya Kimasai kutoka nchi jirani ya  Kenya wakati wakulima hao wakijaribu kuiondoa mifugo ya wafugaji hao  ili isilishe mazao.

Januari  pili  mwaka huu itabaki kuwa kumbukumbu kubwa katika  maisha  ya Protas Sianga Mkazi wa Kijiji cha Kiwanda Wilayani Rombo Mkoani Kilimanjaro baada ya kuambulia kipigo na kunusurika Kifo kutoka kwa kundi la  wafugaji wa jamii ya Kimasai wanaoishi nchi jirani ya Kenya wakati akijaribu kuiondoa mifugo ya wafugaji hao iliyokuwa imevamia shamba lake la Mahindi lenye ukubwa ekari Moja.

Kwa Mujibu wa Maelezo ya wakulima waliozungumza na Star TV wameeleza kuwa wafugaji hao  wameharibu ekari za mazao na sasa wanahofu kubwa ya kukumbwa na baa la njaa. *Kwa undani wa taarifa hii, jiunge nasi katika taarifa yetu ya habari saa mbili kamili usiku.

 

HABARI imeandikwa na Zephania Renatus.

Kuhusu Kisibi Isaya

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *