Wakati kampeni ya usafi wa mazingira za Serikali awamu ya tano zinazolenga kuhakikisha miji na makazi ya watu yanakuwa masafi, katika mji wa Kahama mkoani Shinyanga baadhi ya maeneo yameonekana kukithiri kwa uchafu.

Star Tv imetembelea eneo la Majengo kwenye Halmashauri ya mji huo kujionea utekelezaji wa kampeni ya usafi wa mazingira na kubaini bado hali ya utekelezaji sio nzuri.

Mji wa Kahama  unakuwa kwa kasi kutokana na  kushamili kwa shughuli za kiuchumi na kuwa kitovu cha kibiashara kwa nchi Jirani.

Katikati ya mji mazingira yake yakupendeza lakini kwenye makazi ya wananchi hali sio nzuri maji machafu yanatililika ovyo na kuondoa taswala ya  mji wa Kahama

Wakazi wa maeneo ya majengo sehemu ambayo inaonekana kusahaulika  wanapaza sauti zao kwa mamlaka usika.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa majengo anasema tayari kero hiyo wameifikisha kwenye mamlaka za serikali.

Luhaga Mpina naibu waziri ofisi ya makao wa Rais anasema ni jukumu la Halmashauri za wilaya na miji kusimamia usafi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here