Mshukiwa wa shambulio New York alisifu Islamic State

Mshukiwa wa shambulio New York alisifu Islamic State

- in Kimataifa

news

Waendesha mashtaka nchini Marekani wamemfungulia mashtaka Ahmad Khan Ramani kwa kutega mabomu huko New York na New Jersey mwishoni mwa wiki ambapo mlipuko mmoja ulijeruhi watu 31.

Waendesha mashtaka wanasema kuwa Bw Rahami ambaye ni mhamiaji kutoka Afghanistan, alinunua vifaa na vitu vya kuunda bomu kupitia kwa mtandao na kuandika makala akilisifu kundi la Islamic State.

ia ameshtakiwa kwa kujaribu kuwaua polisi wakati akikamatwa siku ya Jumatatu.

Shirika la ujasusi la marekani FBI linasema kwa lilimchunguza Rahami mwaka 2014 lakini halikumpata na chochote cha kumhusisha na ugaidi wakati huo.

Watu 29 walijeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea mtaa wa Chelsea, New York. Kilipuzi ambacho hakikuwa kimelipuka kilipatikana hapo karibu.

Vilipuzi vingine kadha vilikuwa vimepatikana New Jersey siku za hivi karibuni.

#BBC

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

KUBORESHA ELIMU KWA WATOTO WA KIKE:Serikali yahimiza ujenzi wa mabweni

Makamu wa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hasan