Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Michezo na Burudani / Mtibwa Sugar yaiondosha Polisi Moro kombe la FA

Mtibwa Sugar yaiondosha Polisi Moro kombe la FA

Timu ya maafande wa Polisi Morogoro inayoshiriki ligi Daraja la Kwanza ngazi ya Taifa, imetupwa nje ya michuano ya kombe la Shirikisho, baada ya kushindwa kutamba mbele ya mahasimu wao, wakata miwa Turiani timu ya Mtibwa Sugar, kupitia mikwaju ya Penati.

Mchezo huo ulimalizika kwa timu zote mbili kutoka sare ya goli mbili kwa mbili na kuingia kwenye mikwaju penati, ambapo timu zote ziliweza kupiga penati saba huku polisi Moro wakikosa penati 3 na Mtibwa Sugar wakikosa penati mbili, hivyo kufanikiwa kuendelea raundi inayofuata ya michuano hiyo.

Mtangane huo uliowakutanisha mahasimu hao, umepigwa katika dimba la uwanja wa Jamhuri Morogoro,ambapo mpaka dakika tisini za Mwamuzi zinamalizika, Timu zote mbili ziliweza kutoka sare ya goli mbili kwa mbili na kufanikiwa kuingia kwenye mikwaji ya penati.

Bahati iliweza kuwaangukia wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar, mara baada ya kufanikiwa kushinda mtanange huo kwa kushinda penati tano dhidi ya nne za Polisi Morogoro.

Kufuatia ushindi wa Leo timu ya mtibwa  imefanikiwa kuendelea katika raundi inayofuata ya Michuano ya Shirikisho, huku ikijiandaa na mchezo wa ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya ndugu zao Kagera Sugar, na Polisi Moro wao wakijiandaa kuvaana na Kurungezi, mchezo utakaopigwa Januari 28 huko Mafinga.

Imeandikwa na Jackson Monela.

Kuhusu Kisibi Isaya

Check Also

Kuimarishwa uwanja wa Nyamagana

Mipango ya kuendeleza soka la vijana huenda ikawa na tija endapo tu serikali chini ya …

• SHERIA 17 ZA SOKA: Waamuzi walaumiwa kuziweka

Wakati Ligi Kuu Tanzania Bara, ikifikia tamati ya mzunguko wa kwanza, mashabiki wa soka wametoa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *