Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Mwanafunzi wa KCMC auawa kwa kumchomwa na kitu chenye ncha kali

Mwanafunzi wa KCMC auawa kwa kumchomwa na kitu chenye ncha kali

Mwanafunzi wa mwaka wa tatu taaluma ya Famasia katika chuo cha udaktari cha KCMC mjini Moshi mkoani Kilimanjaro amefariki dunia baada ya kuvamiwa na watu wanaosadikiwa kuwa vibaka na kumchoma kitu chenye ncha kali katika harakati za kumnyang’anya simu.

Tuko hilo la kusikitisha limetokea jana usiku majira ya saa nne katika mtaa wa Neneu karibu na nyumba aliyokuwa akiishi kijana huyo.

 Baneti Materu kijana mwenye umri wa miaka 22 mzaliwa wa Mkoa wa Morogoro..akiwa amebakiza miezi michache ili amalize taaluma yake ya famasia katika chuo cha udaktari cha KCMC maisha yake yanakatishwa kwa kuuwawa kikatili kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali mara tatu maeneo ya tumboni na watu wanaosadikiwa kuwa vibaka wakati akielekea dukani majira ya saa nne usiku.

Huzuni, vilio na majonzi vilitawala katika eneo hilo huku wengi wao wakiwa hawaamini kilichotokea na kusema kuwa tukio hilo siyo la kwanza kutokea.

Wanafunzi wengi wanaosoma katika chuo hicho wamepanga nje ya chuo na matukio ya kuvamiwa na kuibiwa yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara  ambapo tukio hilo  la mauji linazidisha hofu na sintofahamu miongoni mwao.

Mkuu wa Chuo cha Ufamasia KCMC Wensaa Maro  amesema wameshitushwa na kulaani tukio hilo na kuahidi kushirikiana na jeshi la polisi ili kuhakikisha wale wote waliohusika na tukio hilo wanachukuliwa hatua za kisheria

 Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi Mkoa wa Kilimanjaro ACP Wilbroad Mtafungwa amekiri kutokea kwa tukio hilo na polisi inaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wahusika

Licha ya uwepo wa kituo cha polisi katika eneo hilo matukio ya wanafunzi kukabwa, kuibiwa na kuporwa mali zao yameendelea kujitokeza mara kwa mara.

 

 

Kuhusu Joseph Richard

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *