Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Mwekiti, Mtendaji wa kijiji Sambasha Arumeru wasimamishwa kazi 

Mwekiti, Mtendaji wa kijiji Sambasha Arumeru wasimamishwa kazi 

Wananchi wa kijiji cha sambasha wilayani Arumeru mkoani Arusha wameamua kumsimamisha kazi mwenyekiti wa kijiji hicho na mtendaji wake baada ya kutuhumiwa kwa upotevu wa fedha za wananchi ambazo wamekuwa wakitozwa kama michango ya maendeleo ya kijiji baada ya uchunguzi wa kamati iliyoteuliwa kutoa taarifa ya maendeleo.

Baada ya uchunguzi wa kamati iliyoteuliwa na wananchi kubaini makosa  katika taarifa za mwenyekiti na mtendaji wake katika taarifa ya ujenzi wa chumba cha darasa  ambapo kamati hiyo imeweza kubaini upotevu wa sh.milioni nne na laki saba na thelathini na tano elfu.

Mtendaji wa kijiji cha sambasha Lomnyaki Mokolo ambae  hivi sasa  anatuhumiwa  na wananchi kuhusika na upotevu wa   fedha hizo  ambazo wamekuwa wakichanga wananchi hao  kwa ajili ya maendeleo ya kijiji amekiri kuwa  anahusika na kufuja fedha hizo na amesema kuwa atazilipa ndani ya siku saba.

Wananchi wa kijiji cha sambasha wamesikitishwa na uongozi huo kwa ufujaji wa fedha zao na kusema kuwa wamebaini kuwa risiti zilizo husika katika manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa chumba cha darasa ni batili, na diwani wa kata hiyo Lengai Ole Sabaya anasema kuwa wananchi wana mamlaka ya kumwajibisha kiongozi na baada ya siku saba kuisha kabla fedha hazijapatikana atafuata utaratibu wa kisheria.

Wananchi wa kijiji cha Sambasha wamekua wakiulalamikia  uongozi wa kijiji hicho kwa kutosomewa  mapato na matumizi ya fedha zao walizokuwa wakizichanga kwaajili ya maendeleo kijijini hapo kwa takribani miaka saba.

 

 

Kuhusu Joseph Richard

Check Also

Watu wanne washikiliwa Morogoro kwa jaribio la kuvamia kituo cha polisi

Polisi mkoani Morogoro inawashikiria watu wanne wakazi wa Mzumbe wilayani Mvomero, kwa tuhuma za kujaribu …

Maafisa wanne Kigoma wasimamishwa kazi kwa tuhuma za udanganyifu

Mkuu wa mkoa wa Kigoma Brigedia General Mstaafu Emmnuel Maganga ameagiza kusimamishwa kazi kwa Maafisa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *