Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Rais amwapisha Luteni Jenerali Venance Mabeyo

Rais amwapisha Luteni Jenerali Venance Mabeyo

Rais na Amiri Jeshi Mkuu, Dr John Magufuli amemwapisha Lutenia Jenerali Venance Mabeyo kuwa mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi (JWTZ)  pamoja na kuwateua maafisa  wakuu wengine wa jeshi kushika nyadhifa  mbalimbali.

Luteni Jenerali Venance Mabeyo ameshika nafasi iliyoachwa wazi na Luteni Jenerali Ndomba ambaye alistaafu Disemba 31, mwaka jana.

 Mapema Januari 30, Ikulu Jijini Dar Es Salaam Rais John Magufuli amemwapisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi  Lutein Jenerali Venance Mabeyo pamoja na viongozi wengine.

Akizungumzia uteuzi wa maafisa wakuu walioteuliwa, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Jenerali Davis Mwamunyange amesema maafisa hao ni pamoja na Meja Jenerali James Mwakibolwa  ambaye amekuwa Mkuu wa Kamandi ya Jeshi la Nchi kavu  kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Meja Jenarali Salum  Mustafa Kijuu, Meja Jenerali Yakub Sirakwi anakuwa  Mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Gaudence Milanzi ambaye amateuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

Wengine walioteuliwa na Rais ni aliyekuwa afisa mnadhimu katika makao makuu  kamandi  ya Jeshi la Anga Brigedia Jenerali George Ingram  ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Kamandi hiyo, Brigedia Jenerali Jacob Kingu amekuwa  Mkuu wa Shirika la Mzinga.

Brigedia Jenerali Robinson Mwanjela amekuwa Mkuu wa Chuo cha tiba Lugalo, Brigedia Jenerali George Msongole amekuwa Kamanda wa Brigedi ya Tembo na Brigedia Jenerali Sylvester Minja ambaye amekuwa Mkuu wa chuo cha Ukamanda na unadhimu na wote wameshika nafasi zilizoachwa wazi  baada ya waliokuwa wakishika nyadhifa hizo kustaafu.

Wakati huo huo Rais na Amiri jeshi mkuu Dr Magufuli amembakisha jeshini  Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange ambaye alitakiwa kumaliza muda wake January 30 mwaka huu.

Aidha mkuu wa majeshi Davis Mwamunyange ametumia nafasi hiyo kuwapongeza maafisa wakuu wote walioteuliwa.

 

 

Kuhusu Joseph Richard

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *