Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Rais Kikwete awaapisha Wajumbe, Katibu.

Rais Kikwete awaapisha Wajumbe, Katibu.

Na Mwandishi wetu, Dar Es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewaapisha Wajumbe na Katibu wa Tume ya Kuchunguza Operesheni Tokomeza katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu jijini Dar Es Salaam.

Aidha, Rais Kikwete amemwapisha Ofisa Mwandamizi wa Mambo ya Nje Bwana Joseph Edward Sokoine kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Marekani katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Wajumbe wa Tume ya Tokomeza walioapishwa ni Jaji Mstaafu Hamisi Amiri Msumi ambaye anakuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo na Majaji Wastaafu Stephen Ernest Ihema na Vincent Damian Lyimo ambao wanakuwa wajumbe wa Tume hiyo.

Rais kikwete pia amepokea vitabu  milioni 2.5 vya masomo ya sayansi kwa sekondari kutoka nchini Marekani ikiwa ni mwendelezo wa nchi hiyo kuisaidia Tanzania kukabiliana na uhaba wa vitabu na walimu wa masomo ya sayansi.

Balozi Childress amezieleza habari hizo njema kwa Rais Jakaya Kikwete wakati walipokutana kwa mara ya kwanza tangu balozi huyo alipowasili nchini na kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais Kikwete.

Rais pia amekutana na Rais wa Kampuni ya Ujenzi wa Reli ya China Railway Construction Corporation Zhang Zongyan pamoja na Mwenyekiti wa kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation Liu Zhimng kwa mazungumzo ya kuboresha usafiri wa reli nchini.

Rais Kikwete ameondoka nchini jumanne mchana tarehe 24.06.2014 kwenda mji mkuu wa Equatorial Guinea wa Malabo kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Africa – African Union (AU).

Akiwa Malabo, Mheshimiwa Rais Kikwete pia atakuwa Mwenyekiti wa kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa AU kitakachojadili mazingira.

Rais Kikwete na ujumbe wake wanatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki.

Kuhusu admin

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *