Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Rais Magufuli na mkewe washiriki kumbukumbu ya mauaji ya kimbari Rwanda:

Rais Magufuli na mkewe washiriki kumbukumbu ya mauaji ya kimbari Rwanda:

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli jana wameshiriki uwashaji wa mwenge wa matumaini katika kumbukumbu ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda.

Mauaji hayo ya Kimbari yalitekelezwa miaka 22 iliyopita kutokana na migogoro ya ukabila baina ya makabila ya Watusi na Wahutu.

Maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari  ya mwaka 1994 yamefanyika huko Gisozi mjini Kigari nchini Rwanda.

Ikiwa ni moja ya madhumuni ya ziara yake nchini Rwanda Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt  John Pombe Magufuli akiambatana na Mkewe Mama Janet Magufuli ameshiriki  pamoja na Rais wa Rwanda Paul Kagame  katika kuwasha Mwenge  wa matumaini

Akitembelea jumba maalumu lililohifadhi kumbukumbu ya mauaji  ya kimbari Rais Magufuli ameonyesha kusikitishwa na mauaji hayo akisema tukio hilo halipaswi kujirudia tena.

Rais Magufuli ambae alingi nchini Rwanda tarehe 6 mwezi april 2016 ikiwa ni ziara yake ya kwanza ya nje ya nchi toka aingie madarakani  tarehe 5 November 2016 aliondoka mjini Kigari jioni kurejea jijini Dar es salaam.

 

 

Kuhusu Joseph Richard

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *