Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / Rais Shein aongoza Dua ya kumwombea Karume

Rais Shein aongoza Dua ya kumwombea Karume

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dokta Ali Mohammed Shein ameongoza Dua ya pamoja ya kumuombea Rais wa awamu ya kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume aliyeuawa tarehe 7 Aprili, 1972.

Viongozi na wananchi wamejumuika katika ofisi za Chama cha Mapinduzi zilizopo kwenye kisiwa cha Nduwi mjini Unguja eneo alipouawa Hayati Karume na kuzikwa.

Viongozi waliohudhuria wamepata fursa ya kumuombea dua hapo jana na kuweka mashada ya maua.

Hafla hiyo inayofanyika kila mwaka katika mwaka huu imeanza kwa maandamano maalumu yalioandaliwa na vijana wa chama cha mapinduzi na baadae kufuatiwa na duwa.

Mara baada ya kisomo cha kurani viongozi na wananchi wengine walipata fursa ya  kufika katika kaburi la marehemu karume na kumuombea Dua kwa mujibu wa imani mbali mbali za waumini waliofika hapo mara baada ya zoezi la uwekaji wa mashada ya mauwa.

Baadhi ya viongozi waliofika hapo ambao wamepata fursa ya kuzungumza na Star tv wamemzungumzia marehemu karume huku wakieleza mambo muhimu yakuendelezwa alioyaasisi kiongozi huyo.

Hayati karume aliyeongoza mapinduzi yaliowakombowa wazanzibari kutoka utawala dhalimu wa kisultani katika mwaka 1964 ameshatimiza miaka 44 tangu afariki dunia.

 

Kuhusu Joseph Richard

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *