Wednesday , October 18 2017
Mwanzo / Habari / Elimu / RC Mwanza atoa agizo la kusimamishwa kazi watumishi 3 Magu.

RC Mwanza atoa agizo la kusimamishwa kazi watumishi 3 Magu.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza (RC) John Mongella amemuagiza Katibu Tawala wa mkoa huo awasimamishe watendaji watatu wa halmashauri ya wilaya ya Magu kupisha timu ya wataalamu kufanya uchunguzi wa ubadhirifu wa miradi ya Mpango wa Maendeleo ya Sekondari SEDEP wilayani humo.

Watendaji hao ni Mwekahazina wa halmashauri bwana Nickson Itongoro, Simon Nkulu ambaye ni Mhandisi wa ujenzi wa halmashauri na Julian Tarimo Mchumi wa halmashauri.

Dhumuni ni kuona mpango wa maendeleo wa elimu ya sekondari SEDEP wenye lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia ikiwemo ujenzi wa miundombinu unafanikiwa .

Akiwa katika ziara ya kikazi wilayani Magu katika Mamlaka ya mji mdogo wa Kisesa mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella ametoa kauli hiyo katika mkutano wa hadhara wenye lengo la kuhamasisha maendeleo.

Mongella amesema serikali ya awamu ya tano inataka kuona miradi ya maendelo inafanikiwa hivyo timu ya wataalamu ya uchunguzi inayokwenda kuangalia ubadhirifu wa fedha za miradi ya SEDEP wilayani humo na kwamba hivi sasa watendaji hao hawajafukuzwa kazi ila wamesimama kwa kupishauchunguzi.

Katika hatua nyingine Mongela ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya mkoa wa Mwanza amesisitiza suala la ulinzi na usalama katika maeneo mbalimbali mkoani humo huku jeshi la jadi la sungu sungu likitajwa kurejeshwa kwa kasi ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu.

Ziara ya Mkuu wa mkoa wa Mwanza ilikuwa ni ya siku moja wilayani Magu ikiwa na lengo la kuhamisha maendeleo na kujibu kero za wananchi pamoja na kukagua miradi mbali mbali inayotekelezwa na halmashauri hiyo ikiwemo ya elimu.

Imeandikwa na Wilson Elisha.

Kuhusu Kisibi Isaya

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *