RUREFA yapata viongozi wake kwa awamu nyingine.

RUREFA yapata viongozi wake kwa awamu nyingine.

- in Michezo na Burudani

Wajumbe wote wa Kamati Tendaji ya Chama cha Soka Mkoani Rukwa (RUREFA) wamerejea tena kwenye nafasi zao za uongozi kufuatia Uchaguzi Mkuu wa chama hicho uliofanyika mwishoni mwa juma.Msimamizi wa uchaguzi huo James Makunya amemtangaza Blasy Kiondo kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa RUREFA kwa kipindi kingine cha miaka minne, huku msaidizi wake akiwa ni Andrew Ngindo na nafasi ya Katibu ikienda kwa Clement Kanyiki Nsokolo.

Katika uchaguzi huo uliokuwa na wapiga kura kumi na watatu pekee nafasi nyingi zilikuwa na wagombea mmoja mmoja kutokana wajumbe wengi kukosa wapinzani, Baraka Mazengo amechaguliwa kuwa Katibu Msaidizi, Hagai Ambonisye akiwa ni Mtunza Hazina, ilhali Ayoub Nyaulingo akichaguliwa kuwa Mwakilishi wa vilabu katika mkutano mkuu wa TFF, sanjari na John Maholani ambaye anakuwa tena Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF.

Kiu ya Wanarukwa ni kuona maendeleo ya soka lao ambalo yanakwenda mbele baada ya jahazi lake kupoteza ramani kwa takribani miaka kumi na miwili. Je awamu hii wanakuja na mikakati ipi?

Imeandikwa na;

Sammy Jumaa Kisika, Star Tv Rukwa.

Facebook Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

You may also like

Mtibwa Sugar yaiondosha Polisi Moro kombe la FA

Timu ya maafande wa Polisi Morogoro inayoshiriki ligi