Saturday , September 23 2017
Mwanzo / Habari / Biashara na Uchumi / SERIKALI: Tunatambua mchango wa sekta binafsi.

SERIKALI: Tunatambua mchango wa sekta binafsi.

  1. SERIKALI imesema kuwa inatambua mchango mkubwa wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa nchi na kuahidi kuendelea kuimarisha ushirikiano na sekta hiyo ili kuharakisha maendeleo ya wananchi kupitia sekta ya viwanda na biashara.

Hayo yamesema na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, alipokutana na kufanya mazungumzo na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, Bw. Bhaswar Mukhopadhway, Makao Makuu ya Wizara hiyo Jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa uchumi wa nchi unategemea sana sekta binafsi yenye nguvu na yenye utulivu ambayo itachangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kwa njia ya uwekezaji na ulipaji kodi

Hivi karibuni Bodi ya Wakurugenzi ya IMF ilitoa taarifa yake ya mapitio ya mwenendo wa uchumi wa Tanzania na kueleza kuridhika kwake na uimara wa uchumi huo baada ya kutoyumba katika nusu ya kwanza ya mwaka 2016 na kueleza kuwa utaendelea kukua kwa wastani wa asilimia 7 kama ilivyopangwa.

IMEANDIKWA NA BEN MWAIPAJA STARTV, DAR ES SALAAM.

Kuhusu Kisibi Isaya

Check Also

Watuhumiwa TASAF wakamatwa.

Takribani kaya 50 za wilayani Kalambo mkoani Rukwa zimeamriwa kukamatwa mara moja zikituhumiwa  kunufaika na fedha …

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *