Sunday , September 24 2017
Mwanzo / Habari / Kitaifa / TAKUKURU Tabora yaokoa milioni 173

TAKUKURU Tabora yaokoa milioni 173

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) mkoani Tabora, imeokoa kiasi cha shilingi milioni 173 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kuanzia Januari ahdi Disemba mwaka jana.

Katika kipindi hicho,jumla ya mashauri 28 yalifikishwa mahakamani na Jamhuri kushinda mashauri kumi na nne.

Taasisi hiyo mkoani hapa inatekeleza wajibu wake ipasavyo na baadhi ya watu waliochukua pesa wasizostahili wamezirejesha.

 

Pamoja na utendaji kazi wake kupongezwa bado baadhi ya wananchi wanaitaka taasisi hiyo kuongeza jitihada.

 

TAKUKURU Tabora imekuwa ikifanya jitihada za kutoa elimu kwa wananchi na kukutana na makundi mbalimbali kwa lengo la kujitambulisha majukumu yake na kuomba ushirikiano wa wananchi ili kutokomeza rushwa mkoani Tabora.

 

Imeandikwa na Robert Kakwesi – Star TV, Tabora

Kuhusu Kisibi Isaya

Check Also

Makambako yatengewa bilioni 2 za mradi wa maji.

SERIKALI imetenga shilingi bilioni mbili (2) kwaajili ya kusaidia kutatua tatizo la maji katika mji …

Prof. Palamagamba na Majula Bulembo wateuliwa nafasi ya ubunge.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *