Serikali imeendelea kutekeleza ahadi ya kuwahamisha wamachinga kutoka mitaani na maeneo yasiyoruhusiwa na kwenda katika maeneo maalum ambayo wamepangiwa kwa ajili ya kufanyia biashara zao.

Imeelezwa kuwa athari mbalimbali za kuwepo wamachinga wanaofanya biashara kwenye maeneo yasiyoruhusiwa zimeonekana ikiwemo kushuka kwa mapato ya kodi.

Vijana wengi, wamejiajiri kupitia biashara hii ya umachinga, wengine wanasomesha, na wengine wanaendesha maisha kupitia biashara hii, lakini kufanya biashara pekee bila ya kufuata sheria za nchi haitoshi kukupa uhuru.

Na hivyo,ili kuepusha purukashani za kukimbizwa na vyombo vya dola, Serikali inakuja na mpango maalum wa kuwapatia magulio ya kufanyia biashara kwenye Kata mbalimbali za Jiji la Dar Es Salaam.

Wakati huo huo, mkuu huyo wa Wilaya amekutana na wafanyabiashara wa kumbi za starehe ili kuzungumzia mabadiliko ya kanuni ya uendeshaji wa kumbi hizo ambazo zimelalamikiwa na baadhi ya wananchi kuwa ni chanzo cha kelele kwenye makazi ya watu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here